Wednesday, January 25, 2017

KUISHI KWA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU

Kuishi kwa Kuongozwa na Roho Mtakatifu Language Swahili (Wagalatia 5:16-25)

Utangulizi: Hakuna Mkristo mkomavu anayeamini kwamba imani ndio jibu la mwisho la “ni kwa jinsi gani tunapaswa kuishi?” Kufikiri na kutenda vinaendana. Hakuna Mkristo wa dhati anatakayedai kuwa kutembea na Mungu ni jambo rahisi. Wakristo wengi ninaowafahamu kimsingi wanasema, “Ninaokolewa kwa neema pekee. Kwa sababu ya upendo wangu kwa Mungu, ninafanya uamuzi wa kutembea nae na kuyafanya/kuyatenda mapenzi yake.” Nilipojaribu kuwauliza zaidi waliongezea kwa kusema, “Na, kama mtu hatembei pamoja na Mungu, hiyo inaonyesha kuwa hawana imani.” Ama kwa hakika, wale “Wakristo” wanaotumia imani kama kisingizio cha kuishi maisha ya kiovu hawaielewi injili. Lakini, baadaye, nimekuwa nikilitafakari zaidi suala hili kuhusiana na jinsi gani Mkristo anayeokolewa kwa neema anavyopaswa kuenenda katika maisha yake ya kila siku. Hebu tuzame kwenye Biblia yetu na kuona kile ambacho Paulo anatufundisha kuhusiana na maisha ya kila siku! Mzozano/Ugomvi Tunahitaji kupata muktadha, kwa hiyo kwanza kabisa hebu soma kwa haraka Wagalatia 5:16-21. Je, hii inatuambia nini kuhusu neema na kuishi maisha sahihi? (Kama unaishi maisha yenye ubinafsi, maovu, yasiyo makamilifu, hutakwenda mbinguni.) Huyu ni Paulo anayeandika haya! Je, hii inatenda kitu gani kwenye fikra zetu kuhusu neema? (Inamaanisha kuwa mwisho wa neema hauwezi kuwa ni tabia ya kiovu.) Majuma mawili yaliyopita tulijifunza kuwa “mchakato” wa Sara kutimiza lengo la Mungu (kwamba Ibrahim atakuwa na uzao) uliishia kwenye balaa kubwa sana. Je, hakuna tunachoweza kukifanya (au tunapaswa kukifanya) ili tujihusishe kwenye kuishi maisha sahihi? Je, hilo litakuwa ni “mpango wa Sara,” yaani, kosa la “kuhesabiwa haki kwa matendo?” Hebu tuyaangalie haya mafungu kwa undani zaidi. Soma Wagalatia 5:16. Je, inamaanisha nini “kuishi kwa kuongozwa na Roho?” (Ishi kwa mujibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu.) Soma Wagalatia 5:17. Je, hili suala la kuishi kwa kuongozwa na Roho linatendeka? Kama umesema kuwa, “Ndiyo,” je, unaielezeaje kauli ya Paulo kwamba “hamfanyi yale mnayoyataka?” (Inaweza kumaanisha kuwa mnataka kufanya jambo jema, lakini badala yake mnafanya uovu. Pia inaweza kumaanisha mna matamanio ya asili ya kutenda uovu, lakini kwa sababu ya Roho Mtakatifu, badala yake mnatenda jambo jema. Hii maana ya pili inaendana na kile tulichokisoma hivi punde katika fungu la 16.) Soma Warumi 7:21-25. Je, Paulo anazungumzia tu kuhusu watu wabaya? Au, je, anamzungumzia tu wewe na mimi? (Paulo anajizungumzia yeye mwenyewe. Anazungumzia kuhusu Wakristo “wazuri.” Sote tuna asili ya dhambi. Sote tunavutwa kuishi kwa mujibu wa asili hiyo. Tunajikuta tunatenda uovu ambao hatutaki kuufanya.) oma Wagalatia 5:18. Je, hii inamaanisha nini – sina haja ya kuwa na wasiwasi juu ya kile ambacho sheria inakisema? (Haiwezi kumaanisha hivyo, kwani hivi punde tu umesoma kuwa watenda maovu hawatakwenda mbinguni. Hitimisho la pekee la kimantiki ninaloweza kulifikia ni kuwa tuna chaguzi mbili. Tunaweza kuongozwa na Roho Mtakatifu au tunaweza kuongozwa na asili yetu ya dhambi.) Je, hii inapendekeza kuwa kwa namna fulani hivi sheria inahusianishwa na asili yetu ya dhambi? (Soma Warumi 7:8-10. Paulo anasema kuwa sheria inachokonoa tabia ya kidhambi. Hii sio ya kawaida, kwa hiyo tunahitajika kulichunguza hili zaidi.) Kuishi kwa mujibu wa Sheria ijui jinsi ya kuwa na mjadala thabiti wa hili suala bila kuzungumzia dhambi mahsusi. Kwa hiyo, hebu tuzungumzie kuhusu kisa mahsusi kuhusiana na dhambi mahsusi. Soma 2 Samweli 11:1-4. Nimefundisha kisa hiki mara nyingi, nimehubiri kuhusiana nacho. Kama wewe ndiye ungekuwa Daudi, na ukataka kuepuka hii dhambi, je, ni hatua gani za kivitendo ambazo ungezichukua? (Kile ambacho mara zote nimekuwa nikikisema huko nyuma ni kwamba Daudi alikuwa anachukua mfululizo wa hatua kuelekea kwenye dhambi. Baadhi ya hatua zinaweza zisiwe dhambi, lakini bado zilimwelekeza kwenye uelekeo wa dhambi.) Je, hizi hatua mbaya zinaweza kuwa zipi? (a. Kutokwenda vitani na majeshi yake; b. Kumwangalia Bathsheba kwa muda mrefu; c. Kuvutiwa/kupendezewa nae; d. Kutuma apelekewe hata ingawaje alijua kuwa alikuwa ameolewa; na hatimaye kufikia ukomo wa dhambi, e. Kufanya uzinzi.) Kama wewe (namaanisha wewe binafsi) ulitaka kuepuka uzinzi, je, ungeepuka kuchukua hizi hatua? (Ndiyo. Hii inaleta mantiki. Lakini, nadhani kwamba nimekuwa nikifundisha kwa kutumia njia isiyo sahihi. Kiini cha hatua ni sheria. Kiini cha hatua ni uzinzi na jinsi ya kutousogelea kwa ukaribu sana. Kuilenga dhambi na sheria ni njia ya kuhesabiwa haki kwa matendo.” Ninaiangalia asili yangu ya dhambi na ninatafakari jinsi ya kuishinda. Kama Sara, mimi ni mhandisi wa nini cha kufanywa ili kutimiza lengo la Mungu.) Je, onyo la kivitendo la Paulo kuhusu kuhesabiwa haki kwa imani ni lipi? (Halifanyi kazi. Katika Warumi 7:5 Paulo anasema kuwa sheria inaamsha matamanio yetu ya kidhambi. Wagalatia 5:3 inapendekeza kuwa haiwezekani kuitimiza sheria. Katika Wagalatia 5:4 Paulo anaeleza kuwa njia ya matendo inashindwa kwa sababu inamwondoa Mungu kutoka kwenye mpambano.) Je, kuna chochote tunachoweza kukifanya ili kuendeleza tabia zetu wenyewe? Hebu tubaini hilo katika sehemu inayofuatia. . Kuishi kwa mujibu wa Roho oma Wagalatia 5:22-23. Je, ni kwa jinsi gani kuishi kwa mujibu wa Roho kunatofautiana na kuishi kwa mujibu wa sheria? (Unazingatia masuala chanya, hauzingatii masuala hasi. Hauelekezi hatua zako kuelekea dhambini, unaelekeza hatua zako kuelekea kwenye haki.) Hebu turejee kwenye mfano wetu wa msingi wa Daudi. Kama umeamua kuacha kuwafundisha akina Daudi wa siku zijazo kuziangalia hatua zao, kuacha kuziangalia “taa nyekundu” za kimaadili, sasa utakuwa unawafundisha kitu gani? (Vipi kama badala yake tungesema “Mtizamie/mwangalie mkeo. Leta upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi kwenye maisha ya mkeo. Usiziangalie ‘taa nyekundu.’”) Hebu turejee tena kitu fulani tulichojadili juma lililopita. Soma Wagalatia 5:14-15. Hili ndilo lengo la maisha yanayoongozwa na Roho. Je, Daudi angepaswa kuwa anajiuliza kuhusu kitu gani, badala ya kuuliza “Ni hatua gani za kuielekea dhambi (Bathsheba) ninazopaswa kuziepuka?” (Je, ninaweza kufanya jambo gani ili niweze kumfurahisha mke wangu? Je, ninaweza kufanya jambo gani ili niweze kumfurahisha Mungu wangu? Je, ninaweza kufanya jambo gani ili niweze kumsaidia mke wangu? Je, jukumu hili linapendeza mbele za Mungu wangu na mke wangu? Je, hii inakusaidia kuelewa kile anachokimaanisha Paulo anapoandika “kama unaongozwa na Roho, haupo chini ya sheria?” (Roho anauliza, “je, nifanye nini ili niweze kumpenda Mungu na mwenzi wangu?” Sheria inasema, “Je, ninapaswa kufanya nini ili niweze kuuepuka uzinzi?” Lengo ni lile lile – kuwa mwaminifu kwa mwenzi wako. Kama vile Sara na Mungu walivyokuwa na lengo moja – kuwapata wazao kwa ajili ya Ibrahim. Ni mchakato, njia ya kulielekea lengo, linalowatenganisha wale wanaoamini katika kuhesabiwa haki kwa imani na wale wanaoamini katika kuhesabiwa haki kwa matendo.) Wagalatia 5:13 inapotualika “kuwatumikia” wengine, na Wagalatia 5:22 inapotuambia kuwa tunda la kwanza la kuishi maisha yanayoongozwa na Roho ni “upendo,” je, hii inatuambia nini kuhusu kujitazamia wenyewe, ubinafsi, “kutizama kitovu?” (Mambo haya ni makosa.) Je, kuna funzo katika jambo hili kwa ajili yetu kuhusu jinsi ambavyo tunapaswa kutembea na Mungu? (Rafiki, natumaini kwamba unaweza kuona kuwa kuitazamia sheria, kuzitazamia “taa nyekundu” ni kujitazamia mwenyewe. Je, ninaendeleaje? Kutazamia kumpenda Mungu na wenzi wetu na wengine kunafikia kwenye swali, “Je, vinaendeleaje? Je, ninavifurahisha?) Soma Wagalatia 5:24. Je, njia yetu ya kukabiliana na asili yetu ya dhambi inapaswa kuwa ipi? (Tunataka ife! Je, unaweza kuona tena kuwa ni makosa kwa kiasi gani kuzitazamia asili zetu za dhambi na kupima vipimo vyake kuielekea dhambi?) oma Wagalatia 5:25. Kama unataka kuendana hatua kwa hatua na mwanadamu mwingine, je, unahitajika kufanya nini? (Angalia jinsi mtu huyo alivyotembea.) Je, inamaanisha nini kuendana “hatua kwa hatua” na Roho? (Kumwangalia Mungu wetu na kile kinachompendeza.) Hebu turejee tena Wagalatia 5:24-25. Je, sheria bado ni ya muhimu? (Ndiyo. Kama Wakristo “wasio wakomavu” sheria inatufundisha kuwa tunamhitaji Mwokozi. Lakini, mara tunapoupata huo ujumbe, basi hatupo tena chini ya uangalizi wa sheria. Hatujiangalii tena sisi wenyewe, kujipima wenyewe dhidi ya sheria. Badala yake, tunamwangalia Mungu, huku tukiwa tukiongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu ili tuweze kumpendeza Mungu. Basi kinachomiminwa maishani mwetu ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi.) Kama unajiona kuwa wewe sio mvumilivu, je, unapaswa kulifanyia hilo kazi? (Hapana! Hauiangalii dhambi. Usiyaangalie matendo, na kwa ujumla kuenenda kama Sara alivyofanya. Kwa uwezo wa Roho wa Mungu, badala yake zingatia kumpenda mtu ambaye huna uvumilivu nae. Hiyo ndio njia ya neema. Hiyo ndio njia ya kuhesabiwa haki kwa imani.) Soma Wagalatia 5:26. Kwa nini tuwe na majivuno kwa kuishi maisha sahihi? (Kama lengo ni kwa jinsi gani tunaishinda dhambi, na kama hatuko macho sana, hili linaweza kutokea. Kama lengo letu ni kumpenda Mungu na wale wanaotuzunguka, kamwe hili haliwezi kutokea.) Rafiki, natumaini kwa sasa unaweza kuona kwamba haki kwa imani sio tu kuwa inatuokoa kwa neema ya Mungu, bali pia inatuambia jinsi ambavyo tunapaswa kuishi kila siku. Je, utaamua hivi sasa kuacha kuangalia na kuzitazamia “taa nyekundu” na kuanza kuangalia jinsi ya kumpenda na kumfurahisha Mungu?

MAISHA NA NENO LA MUNGU
WHATSAPP GROUP

Jih

Kati ya maadui zako wa imani wanaoweza kukufanya ukose mema na kupoteza muujiza wako wa kwanza kabisa ni mashaka. MASHAKA JUU YA KILE MUNGU ALICHOSEMA (AHADI) Yakobo 1: 6 Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku. 7 Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu cho chote

IJUE VITA YAKO

IJUE VITA YAKO

Kati ya maadui zako wa imani wanaoweza kukufanya ukose mema na kupoteza muujiza wako wa kwanza kabisa ni mashaka.

MASHAKA JUU YA KILE MUNGU ALICHOSEMA (AHADI) Yakobo 1: 6 Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku. 7 Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu cho chote kutoka kwa Bwana. 8 Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote. Ni shida mtu kupokea chochote ikiwa ana mashaka na uaminifu kwa Mungu. Mashaka yanamfanya Mungu awe kigeu geu au tapeli. Mashaka yanamdhalilisha

Mungu. Mungu anakuwa kama vile anasema ovyo, hajui anachosema na wala hakimaanishi. Maneno ya Mungu si maneno ya mwendawazimu, ni maneno imara yasiyotanguka. Waebrania 6: 13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi Yake, kwa kuwa hakuwepo mwingine aliyekuwa mkuu kuliko Yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake, aliapa kwa nafsi Yake, 14 akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” 17 Kwa njia hii, Mungu alipotaka kuonyesha kwa udhahiri zaidi kwa warithi wa ile ahadi ile asili ya kutokubadilika kwa ahadi Yake, aliithitibisha kwa kiapo. 18 Mungu alifanya hivyo, ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi Yake na kiapo Chake, ambavyo kwa hivyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia, tuwe na moyo mkuu kulishika lile tumaini lililowekwa mbele yetu. Mungu alipompa Ibrahim ahadi aliweka na kiapo. Neno la Mungu linaonyesha alitaka kuwapa wale watakaomwamini uhakika kuwa anaweza kufanya yote aliyoahidi. Hivyo kwa mambo mawili yasiyoweza kubadilika yaani ahadi na kiapo sisi tupate faraja sisi tuliomkimbilia Mungu kuwa faraja yetu. Kile Mungu anachosema amefanya tayari amefanya. Kama anasema “ kwa kupigwa kwake (Yesu) mliponywa.” Ina maana ni kweli kabisa tulikwisha ponywa mbele za macho ya haki ya Mungu. Hakuna ugonjwa wowote wenye uwezo wa kutung’ang’ania ikiwa tumesimama katika ukweli huu. Hapa shetani atakachojaribu kufanya ili aweke magonjwa juu yetu ni kututia mashaka juu ya uponyaji huu. Shetani ataleta mawazo ya kuona kama haiwezekani kuwa tayari tumeponywa. Ataleta mawazo ya kuahirisha jambo hili. “Labda siku za mbele upako utakapoongezeka kanisani bila shaka utaponywa. Mungu yupo siku moja atakusaidia.” Haya ni mawazo ya uongo toka kwa shetani. Ukweli unabaki vile vile kwa atakaye uamini “ kwa kupigwa kwake (Yesu) mliponywa.” Wakati umefika kwa mwenye mashaka kuyatumia mashaka yake vizuri. Hebu tumia uwezo wako wa kutia shaka kwa kutilia mashaka mashaka yako. Mtilie mashaka shetani. Kwa nini umtilie mashaka Bwana Yesu na maneno yake na ushindwe kumtilia mashaka shetani na mawazo ya mashaka anayokuletea? Jisemee kama Daudi “ Sitakufa bali nitaishi” “Aliye pamoja name ni mkuu, kuliko yeye aliye katika dunia”. TARAJA Waebrania 11: 1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni udhahiri wa mambo yasiyoonekana.” Imani ni sasa. Taraja huonekana kama rafiki mzuri. Taraja au tumaini ni kama chui mwenye madoa doa na sura nzuri. Tena kucha zake huzificha ndani ya mfuko wa mkono wake. Lakini ukweli ni kuwa chui ni hatari sana. Taraja huhairisha muujiza wako na kuupeleka katika tarehe za mbele zisizojulikana. Hupotezi tumaini la kupata suluhisho toka kwa Mungu, lakini taraja husema sio leo. Imani inasema ni leo. Mungu anajitambulisha kwetu kuwa yeye ni Mungu wa leo. Ni NIKO AMBAYE NIKO. Kutoka 3:14 Marko 11:23-24. 24 Kwa sababu hiyo nawaambia, yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea nayo yatakuwa yenu. Huwezi kupata isipokuwa unayo. Biblia husema ili uweze kupokea kitu toka kwa Bwana wakati unaposali uamini kuwa kile kitu ulichokiomba umekipokea kwanza. Ndani ya moyo wako uwe na uhakika kuwa tayari jambo uliloomba umepewa. Kwa imani ushikilie kile kitu mkononi. Uwe na uhakika kuwa unacho. Ndipo biblia husema kitakuwa chako. Utakuwa nacho. Kwa maneno mengine ni kuwa ushinde mashaka juu ya kumiliki kile kitu na pia usiweke umiliki wa hicho kitu siku za usoni. Usiseme Mungu akipenda kitu hiki nitakipata. Useme namshukuru Mungu amenipa kitu hiki na kile. Labda rafiki fulani atasema Oh vizuri sana wewe ni mtu mwenye bahati, je kiko wapi kitu unachoniambia tayari umekipata? Hapo usiseme “kusema ukweli bado sijakipata.” La mwonyeshe ahadi ya Mungu, sema rafiki Mungu amenipa afya yangu pale Yesu alipopigwa mijeledi. Afya ninayo sasa hebu angalia hapa katika 1 Petro 2:24. Namshukuru Mungu sana kwa mapigo yale niliponywa! Mfano rahisi ni Mariamu na Yesu. Yohana 11: 21 Martha akamwambia Yesu, ‘‘Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa. 22 Lakini sasa ninajua kuwa cho chote utakachomwomba Mungu, atakupa.’’ Martha alikuwa anaamini katika uwezo mkuu wa Bwana Yesu, na alijua siri ya nguvu ya maombi aliyo nayo Yesu. Martha ni picha ya wakristo. Watu wanajua Yesu ana uwezo mkuu. Tena watu wanajua siri kuu katika nguvu ya maombi 23 Yesu akamwambia, ‘‘Ndugu yako atafufuka.’’ Bwana Yesu alipoona kauli imara ya Martha juu ya nguvu zake na uwezo wake akamfunulia kusudio lake pale. Hii ni ahadi isiyoweza kutanguka kutoka kwa Bwana Yesu. Tena haina masharti yoyote. Ni ahadi ya moja kwa moja. Ahadi zingine zina masharti, ukifanya hivi itakuwa hivi. Lakini ahadi hii haina sharti lolote. Yesu yupo tayari kutenda jambo kubwa hapa. 24 Martha akamjibu, ‘‘Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.’’ Unaweza kuona mwitikio wa Martha kwa azma na kusudi la Yesu. Yesu amekwisha weka wazi lengo lake. Martha anapingana na Bwana Yesu kwa kujifanya wa kiroho. Anahairisha muujiza wa ndugu yake kufufuka. Yesu una nguvu lakini hili la Lazaro kufufuka si la sasa. Itakuwa siku ya mwisho. Hili ni taraja au tumaini. Tumaini linaondoa mwujiza sasa na kuupeleka siku ya mwisho. Unaweza kusema haina madhara lakini itabidi Lazaro abaki kaburini hadi wakati huo. Yesu anamwambia Martha huko ni mbali sana. Mimi ndiye huo ufufuo na uzima unaousubiri siku ya mwisho. Niko hapa pamoja nawe sasa hivi, je ni lazima tusubiri siku ya mwisho? Kama unaamini kuwa Lazaro atafufuka na mimi ufufuo na uzima niko hapa tunasubiri nini? 25 Yesu akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye Mimi, hata akifa atakuwa anaishi 26 na ye yote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?’’ Unaweza kuona watu wengi wameahirisha miujiza ya Mungu katika maisha yao kwa kusogeza tarehe mbele. Inasikika kama wako kiroho sana. Wanasema najua tu Mungu mwenyewe ndiye atakaye nisaidia. Sina mashaka iko siku Mungu ataniponya. Lakini bado hiyo sio imani. Imani ni sasa, inapokea na kumiliki leo. Kama watu wengi ambao wamengoja kwa uvumilivu miujiza yao wangerekebisha kidogo imani zao ni kuziweka katika hali ya sasa wangepokea haja zao. Imani ni sasa.

Bwana mwenyezi Mungu anaweza kufanya mambo yote hakuna lisilo wezekana Luka 1:37

Mungu anaskia maombi ya watoto wake anatuamuru kuomba na ameahidi kuskiliza wakati tunaomba.

Katika shida yangu nalimwita Bwana na kulalamika Mungu wangu akaskia sauti yangu.kilio changu kikaingia maskioni mwake zaburi 18:6)

Mpendwa wa Mungu naomba utambue kuwa kuomba kuna nguvu nyingi ya kujusaidia unaposhindwa kuomba ujue umeingia kwenye vita ya kukurudisha nyuma.

Mungu akuinue mpendwa katika Bwana.

By Stella mbogela.

6Ngoja nikuonyeshe kitu kingine. Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. (GAL. 5: 16 - 17). Maandiko hapa yapo wazi kuwa tukienenda kwa Roho hatutatimiza kamwe tamaa za mwili. Unapokoka tamaa za mwili hazifi. Ila unazidhibiti kwa kuenenda kwa Roho. Huwezi kuenenda kwa Roho kama roho yako wewe ni dhaifu. Kinachofanya roho yako iwe na nguvu ni kuukulia kwako wokovu na kuukulia kwako wokovu kunategema mafundisho sahihi unayopata na jitihada binafsi za kinidhamu za usomaji wa neno. Wengi wanahangaika na kutimiza tamaa za miili yao kwa sababu hawaenendi kwa Roho na wanashindwa kuenenda kwa Roho kwa sababu roho zao ni dhaifu na ni dhaifu kwa sababu hawajaukulia wokovu na hawajaukulia wokovu kwa sababu hawajayatamani maziwa ya akili yasiyoghoshiwa ambayo ni mafundisho sahihi ya neno la Mungu na usomaji binafsi wa neno la Mungu. Kukua ndiko kunakoongeza nguvu ya roho zetu na kurahisisha kuenenda kwetu kwa Roho. Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli. (LK. 1: 80). Kwa kadiri unavyokua ndivyo unavyoongezeka nguvu rohoni na inakuwa rahisi kuyaishi maisha ya kuenenda kwa Roho maana roho iliyokua ni rahisi sana kumwitikia Roho Mtakatifu. Ngoja nikuonyeshe andiko lingine: mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. (EFE. 4:22 - 24). Katika andiko ambalo tumetoka kunukuu tunaambiwa tuvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kufuata tamaa zenye kudanganya. Kuvua ni mchakato ambao unawezeshwa na kufanywa upya roho ya nia zetu kwa njia ya mafundisho sahihi ya neno la Mungu na usomaji wa neno katika maisha ya mwamini. Hatuishii tu kwenye kuuvua utu wa zamani bali pia tunaenda hatua moja zaidi ya kumvaa mtu mpya aliyeumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. Huu mchakato wa kuuvua utu wa zamani na kuuvaa utu mpya ndo unaitwa kuongoka na unawezekana tu kama tayari umeokoka. Lakini pia tuwe makini kujua kuwa kuongoka hakutokei tu kwa sababu umeokoka. Kuongoka kunatokea kwa sababu kuna hatua za makusudi unazichukua kama ambavyo tumeona kwa sehemu kwenye hili somo la leo. Tuangalie tena andiko lingine. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. (EFE. 4:15). Kwa kadiri tunavyoishika kweli (ambayo ni neno la Mungu, na hiyo twaishika kwa kuiishi, huku tukisukumwa na upendo wetu kwa ajili ya Bwana), tunakua hata kumfikia Yeye Yesu katika yote kimwenendo na kitabia. Huku sasa ndo kuongoka. Nimalizie somo la leo kwa andiko lingine. Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho. (2 KOR. 3: 18). Uso usiotiwa utaji unaozungumziwa kwenye andiko tulilonukuu ni uso ambao haujazibwa kuona kile ambacho neno la Mungu linatufundisha. Kwa kadiri tunavyoelewa kile ambacho neno la Mungu linafundisha hilo litaonekana zaidi katika maisha yetu ya kimwenendo na kitabia na itapelekea sisi kubadilishwa ambako ndiko kuongoka kwenyewe. UMEBARIKIWA MNO, YESU AKUTUNZE.

KUOKOKA NA KUONGOKA

KUOKOKA NA KUONGOKA Bwana Yesu Asifiwe. Neema na Amani zizidishwe kwako. Napenda nizungumze na wewe kidogo. Ukiangalia kwa haraka haraka unaweza ukaona maana ya hivi vitu viwili KUOKOKA na KUONGOKA.vipo sawa lakini havipo sawa hata kidogo. Yesu siku moja akizungumza na wanafunzi Wake aliwaambia: Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. (LK. 22:31, 32). Katika hayo maandiko hapo juu inaonekana wanafunzi wangepitia mahali pagumu lakini Yesu akawa amemwombea Petro ili imani yake isitindike au isishindwe na akamwambia atakapoongoka, au kwa maneno mengine atakapobadilishwa kutoka kwenye hiyo hali kurejea kwenye hali ambayo alitakiwa awe nayo awasaidie wengine. Tunapozungumzia kuokoka tunazungumzia kutolewa dhambini na Yesu kwa njia ya muujiza wa kuzaliwa mara ya pili. Ni kuhamishwa toka kwenye ufalme wa giza kuja kwenye Ufalme wa Mwana wa Pendo Lake. Ni kutoka gizani kuja nuruni. Kuokoka kunazungumzia zaidi kuhamishwa. Kuongoka ni kitu ambacho kinaanza kutokea baada ya kuokoka. Ni badiliko ambalo linaanza na kuendelea ndani ya mtu baada ya kuokoka ili kumfanya azidi kufanana na asili ya uamuzi ambao ameuchukua wa kumpa Yesu maisha Yake. Tuangalie maandiko mawili matatu tuweze kuelewa kidogo hiki kitu. Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. (MT. 11:28 - 30 ). Kwenye mistari ambayo ndo tumetoka kusoma kuna vitu viwili vinazungumziwa kwenye hii mistari. 1. Kuja kwa Yesu ambako ndo kuokoka kwenyewe. 2. Kujifunza kwa Yesu ambako ndiko kutakakosababisha badiliko ambalo ndo kuongoka kwenyewe. Wengi wakishaokoka wanafikiri ndo mwisho wa kila kitu wakati kuokoka ni mwanzo tu wa safari. Baada ya kuokoka lazima ujifunze namna mpya ya kuishi kwa kujifunza maneno ya Mungu. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. (MT. 28:19 - 20 ). Yesu alipowaagiza wanafunzi Wake wakawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi aliwapa vitu viwili vya kufanya: 1. Wakawabatize ambako ndiko kuokoka maana sehemu nyingine maandiko yanasema aaminiye na kubatizwa ataokoka. 2. Kuwafundisha kushika yote aliyo waamuru ambako ndiko kutazaa kuongoka au badiliko la kitabia. Wengi wamefadhaishwa na kukatishwa tamaa na wokovu maana hawaoni badiliko la kitabia baada ya kuokoka wasijue kuwa wokovu huleta badiliko la hadhi (status) na mafundisho ndiyo huleta badiliko la kitabia na mwenendo. Kwa kadiri mtu unavyojitoa kwenye mafundisho na kulisoma neno la Mungu unajengwa kwenye utu wako wa ndani ili uweze kuanza kubadilika kitabia na kimwenendo. Embu tuangalie andiko lingine. Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. (YN. 8:31 - 32). Katika andiko ambalo ndo tumetoka kusoma tena tunaona kuna vitu viwili vinazungumziwa: 1. Kumwamini Yesu ambako ndiko kuokoka. 2. Kuendelea katika neno Lake ambako ndiko kunaleta mabadiliko ya kitabia na kimwenendo ndani ya mtu ambako ndo kuongoka kwenyewe. Wengi wamepitia hatua ya kwanza ya kuokoka lakini kwa sababu hawakuendelea katika neno Lake kwa njia ya mafundisho na usomaji wa neno hawajaanza kuona mabadiliko ya hatua ya pili. Hatuwezi kuwekwa huru kimwenendo na kitabia kama tusipoendelea kwenye hatua ya pili ambayo ni ya kuendelea katika neno Lake. Wengi wamekatishwa tamaa na kutokubadilika kwa tabia zao baada ya kuokoka kwa sababu hakuna hatua za makusudi ambazo wanazichukua kujenga mazingira ya badiliko hilo au wamejenga lakini hawajaipa muda wa kutosha wa kuanza kusababisha hilo badiliko. Kuna kuokoka na kuna kuukulia wokovu. Kuokoka ni tukio ambalo atokana na uamuzi wa kunfanya Yesu Bwana.na Mwokozi wa maisha yetu. Kuukulia wokovu ni mchakato na huo mchakato ndo unaitwa kuongoka. Tuangalie tena andiko lingine. Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; (1 Petro 2: 2). Watoto wachanga waliyozaliwa sasa  ndo hao waliyookoka na tukishaokoka tunatakiwa kuyatamani maziwa ya akili yasiyoghoshiwa ambayo ni mafundisho sahihi ya neno la Mungu na usomwaji wa neno. Usipokuwa msomaji wa neno na mhudhuriaji wa mafundsisho huwezi kuukulia wokovu na usipoukulia wokovu huwezi kuona badiliko la kitabia na kimwenendo maishani mwako. Hapo ndo wengi walipokwama.

Tuesday, January 24, 2017

Jifunze kuishi maisha ya kusamehe

Katika maisha tunayoishi Hapa Duniani kwakuwa tu wapitaji basi na makwazo hayana budi kutokea  ila tunajifunza, kama vile ambavyo mtu Mwema anavyoweza kujifunza ubaya akawa Mtu muovu ndivyo ambavyo mtu mubaya anavyoweza kujifunza wema na akawa mtu mwema inategemea unajifunza kwa nani, kwa Mungu au kwa Shetani Mwenye sifa ya kusamehe dhambi Maandiko yameweka wazi ni Yesu kristo peke yake hivyo ni Vema tukajifunza kwake,  Mathayo 11:29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Ø  Utu wema Ø  Upole Ø  Unyenyekevu wa Moyo Ø  Kupata raha  nasfsini tunajifunza kwa Yesu kristo, Ø  Mungu anataka ujifunze leo itakusaidika ikiwa utakuwa tayari kujifunza, Ø  utayari wako ni wa muhimu Sana  ruhusu mabadiliko yaanzie kwako,leo   Watu wengi sana wanaokosewa  Wanasamehe sana lakini kusahau tukio au kwazo lililosababisha msaha utoke  ni vigumu sana kusahau, Na hili ndilo jambo linalowatesa kila inapoitwa leo,  kutosahau kosa baada ya kusamehe nikuendelea kuutunza Ugonjwa  badala ya kutibu, Hata kanuni ya Mungu anaanza kutusamehe kabla hajatuponya magonywa yetu,

JIFUNZE KUSAMEHE NA KUSAHAU

Yeremia 1:4  Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.  Tangu tumboni Mwa mama mzazi  ndipo tunapoanzia kujifunza Mambo mbali mbali,kwa kuhisi hali ya mazingira tunayotarajia kuja kuishi,  Tunapofika ulimwenguni tunaendelea kujifunza kwakuhisi,kuona,kusikia, kila kitu, kutofautisha ni pale utapopata Neema ya Mungu kwakuwa tunaishi katika falme mbili, unapokuwa bado tumboni unaishi katika falme tatu, Mungu,mzazi,shetani japo falme kuu bado inabaki kuwa ya Mungu Falme kuu mbili  zinazofanya kazi hapa Duniani, Ø  Ufalme wa Mungu- (Nuru) Ø  Ufalme wa Muovu-(Giza) Ni vizuri ukafahamu hilo kwanza kabla ya mengineyo Mengi ,Ufalme wa Mungu Unasimamiwa na Mungu Mwenyewe Katika Utatu Mtakatifu Mungu Baba,Mwana,na Roho Mtakatifu, katika mambo yote matakatifu, Ufalme wa Muovu (Shetani)nao unasimamiwa na Shetani mwenyewe na majeshi yake,Katika mambo maovu yote, Falme hizi zote zina fanya kazi katika Ulimwengu wa ki-Roho na kujidhihirisha katika Ulimwengu unaoonekana kwa Macho ya Damu na nyama, kwa sababu Maalumu, na Hizi falume zinashindana kila wakati,  Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Mema yote au Mabaya yote  yanafanyika kupitia Falme hizi nilizozitaja hapo juu, Mwanadamu asipotumika katika Mema basi atatumika katika Mabaya,asipomtumikia Mungu atatumikishwa na Shetani, usiposababisha makwazo utasababishiwa,

MAISHA NA NENO LA MUNGU

Acha Neno la Mungu Liangaze Barabara Yako “Neno lako ni . . . nuru kwa barabara yangu.”—ZABURI 119:105. 1, 2. Ni katika hali gani neno la Yehova litaangaza barabara yetu? NENO la Yehova litaangaza barabara yetu tukiliruhusu lifanye hivyo. Ili kunufaika na nuru hiyo ya kiroho, lazima tujifunze kwa bidii na kufuata shauri la Neno la Mungu lililoandikwa. Hilo tu ndilo litakalotuwezesha kuwa na hisia kama hizi za mtunga-zaburi: “Neno lako ni taa ya mguu wangu, na nuru kwa barabara yangu.”—Zaburi 119:105. 2 Sasa tuzungumzie Zaburi 119:89-176. Mistari hiyo ina habari nyingi sana zilizopangwa katika beti 11, nayo inaweza kutusaidia kudumu katika barabara inayoongoza kwenye uzima wa milele.—Mathayo 7:13, 14. Kwa Nini Ulipende Neno la Mungu? 3. Zaburi 119:89, 90 inaonyeshaje kwamba tunaweza kulitegemea neno la Mungu? 3 Tukilipenda neno la Yehova tutakuwa imara kiroho. (Zaburi 119:89-96) Mtunga-zaburi aliimba: “Mpaka wakati usio na kipimo, Ee Yehova, neno lako limesimama mbinguni. . . . Umeiweka dunia imara, ili ipate kuendelea kusimama.” (Zaburi 119:89, 90) Kwa neno la Mungu, yaani, ‘sheria zake za mbingu,’ jua, mwezi, na nyota husonga katika mizunguko yake pasipo kugongana, nayo dunia imewekwa imara milele. (Ayubu 38:31-33; Zaburi 104:5) Tunaweza kulitegemea kila neno linalotoka katika kinywa cha Yehova kwa sababu kila asemalo “hakika litafanikiwa” katika kutimizwa kwa kusudi lake.—Isaya 55:8-11.

Monday, January 23, 2017

JE UNAMJUA MALAIKA WAKO?

Bwana YESU asifiwe,
Napenda leo tujifunze kuhusu malaika.

Umesikia sana neno hili malaika, je unajua ni nani huyu malaika?

Basi fuatana na mimi katika hili somo uweze kupata ufahamu wa  malaika ni nani hasa.


NINI MAANA YA MALAIKA?

Kwenye lugha ya kingereza malaika anaitwa "angel" ila hilo neno limetolewa kwenye neno la kigiriki linaloitwa "angelos" ambalo kwa tafsiri yake halisi ya kingereza ni "messenger".
Kutokana na tasfiri hio basi tukija kwenye lugha yetu tunaona kua lina maanisha "mjumbe"

Mjumbe ni yule ambaye amebeba ujumbe wako au wa kitu chochote, kwahio tunapata maana yake kua malaika ni mjumbe kwahio kwa lugha rahisi na nyepesi malaika wako ni yule aliyebeba ujumbe wako.

Ukisoma biblia yako vizuri utaona kua popote malaika alitokea alikua na ujumbe wa mtu.


KUTOKA 23:20-22

"Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.

 Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.

Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao."

 

Ni hivi kutokana na hilo neno ukiangalia ufunuo uliopo ndani yake ni hivi:-
  1. MCHUNGAJI
  2. MWALIMU
  3. MTUME
  4. NABII
  5. MUINJILISTI    
Hawa wote kama watumishi walioko mbele zako ambao wamepewa neno la kukufundisha hawa ndio malaika wako.

Ambaye yuko mbele yako kama kiongozi wako wa kiroho ambae MUNGU kamueka mbele yako huyo ni malaika wako.

Ni mjumbe wako maana amebeba ujumbe wako toka kwa MUNGU.

Anaposema anamtuma malaika aende mbele zako anamaanisha atamtuma mtumishi wake aje mbele zako. Akuonyeshe, akufundishe neno la MUNGU ili ujue namna ya kukaa na MUNGU  ili akufikishe kwenye kusudi.
MUNGU anazidi kuhimiza msikilizeni akimaanisha msikilize sana kiongozi wako wa kiroho tii kile anachokufundisha.

BONYEZA KWENYE LINK HII UJIUNGE KWENYE GROUP LETU LA WHATSAPP
MAISHA NA NENO LA MUNGU WHATSAPP GROUP