MADHARA YA KUKOSA AU KUONDOLEWA KWA MAARIFA YA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO
LUKA 11:52
52 Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.
BWANA YESU APEWE SIFA SANA SANA
Neno ole ni neno linaloashiria kuwepo kwa madhara juu hilo lililofanyika au fanywa
Wanasheria wa Musa walijikuta wanaingiza sheria ambazo azitoi maarifa kwa watu juu ya kumjua Mungu wao ,waliweka maarifa ambayo hayakuwafanya wajue ukweli juu ya Mungu wao badala yake wakawa wanaondoa hali ya kuwafanya wawe karibu na makini na kweli ya neno la Mungu ,waliondoa njia ya kupata maarifa ya kumjua Mungu wao lakini pia sheria hizo hizo ziliwaharibu na wao pia walipozisikia ,maana ziliondoa maarifa ya kumjua Mungu kwa watu na kwao pia ,kwahiyo ziliwafunga wote watungaji na wasikiaji pia
Ukisoma ile Danieli 1:1-5 ,Mfalme Nebukadreza alijitafutia vijana wenye maarifa ni mmoja wa vijana aliowachagua wasimame mbele zake kutoka katika taifa la Israeli Daniel alikuwa n mmoja wapo kabisa sasa angalia ile Daniel 6:1-17👉Utaona kuwa mawaziri na maliwali waliona wivu juu ya Danieli na wakamtafutia mashitaka ili kumvuruga katika maisha yake na ili kumvuruga walitaka kutumia sheria ya Mungu wake ,na sheria ya Mungu ni utaratibu wa Mungu juu ya mtu ambao uwa unamfanya yule mtu kumjua na kumuelewa Mungu wake na kufanya yampendezayo kwahiyo wakaona kuwa ili kumkosesha lazima tuingize sheria ambazo zitamfunga katika kumjua na kumfuata Mungu wake maana waliona chanzo cha mafanikio yake n maarifa au ufahamu alionao ndani yake juu ya Mungu wake ivyo wakabadili sheria ya nchi na katika hiyo sheria wakaweka na kipengele cha kumfungia Danieli asiweze kuendelea kumtafuta Mungu wake arudi nyuma na kumkosea Mungu wake lakin Danieli alikataa kukaa katika hiyo sheria kabisa na Mungu alimpigania ,unakuta mtu yuko kanisani alafu ghafula mambo yanabadilika pale anaona watu wamemuinukia au kama hawampendi anarudi nyuma au mapito yamekuwa magumu juu yake anarudi nyuma na kuhacha kumtafuta Mungu na wokovu anahacha ,ndugu hapo unakuwa unaondoa ufunguo wa maarifa mwenyewe ,Danieli aligoma akaendelea na Mungu wake ,hakuacha maarifa ya kuendelea kumuomba Mungu ,aliendelea na Mungu akampigania hakuondoa ufunguo wa maarifa kwa sababu ya sheria ya mawaziri na wakubwa
Swala la kuombea sheria zinazotungwa juu ya nchi n muhimu sana kwa sababu ujui n kipengele gani kitakubana na kukuondolea maarifa ya Mungu wako ,kule marekani kipengele cha kuruhusi ushoga na usagaji kwenye sheria yao kimeondoa maarifa ya kumjua,kumuhofu ,kumuheshimu ,kumpenda Mungu kabisa ,ufunguo uo mbaya wa sheria umewafungia wengi kumjua Mungu na kumuishia Mungu na ubaya wa sheria hizo uwezi kutunga na kuzipitisha bila ya kwanza kukuathiri na wewe mtungaji lazima wapitishaji wawe nao wao wanafanya hayo ya makufuru kwa Mungu na hata kwa Danieli wale waliotunga ile sheria juu ya Danieli waliingia kwenye moto wenyewe
Hosea 4:6-9
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ;kwakuwa wewe umeyakataa maarifa ,mimi nami nitakukataa wewe ,usiwe kuhani kwangu mimi ;kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako ,mimi nami nitawasahau watoto wako "
Sheria ya Mungu wako yaani ule utaratibu wa Mungu wako uo ndio wenye kufungua maarifa ya Mungu maishani mwako ,ukikosa huo sahau kuwa na maarifa ya Mungu na maangamizi yatakuwa juu yako
Ndio maana tunashauriwa tujae maneno ya Mungu ndani yetu na yakijaa yatatupa kujua Mungu wetu anataka nini na yukoje na hatutaweza kuangamia kabisa
Ukisoma ile 1Wakor12:4-12
Liko neno la maarifa ambalo uwa linaleta maarifa kwa watu wa Mungu na hilo neno linahachiwa kwetu kama tukikaa katika kumpendeza Roho Mt ,anatupa ili litupe maarifa ndani yetu na kujua namna ya kuenenda na la kufanya mbele za Mungua
No comments:
Post a Comment