Friday, July 14, 2017

MAPAMBO

Wana wa Mungu,Bwana Yesu Kristo asifiwe.Habari za uzima wapendwa.
Ni matumaini yangu kwamba wewe ni mzima wa afya tele katika Bwana.

Nakukaribisha mpendwa tusemezane  na tujifunze neno la Mungu.

            Ujumbe: M A P A M B O
                         ===============

Tutambue kwamba kuna aina mbalimbali  za mapambo wapendwa.
Leo nakuletea hizi hapa.

Neno Mapambo
-------------------------: Ni jumla ya urembo uliyowekwa ili kupendezesaha mwili au sehemu yoyote ile,au kupendezesha kitu Fulani.

Aina ya Pili ya Mapambo
-------------------------------------: Ni fedha au Mali inayolipwa na mwanaume kwa wazazi wa mwanamke anayetaka kumwoa,yaani mahari.

Lakini neno Pambo
-----------------------------Ni kitu cha kupendezesha au kitu cha kuongeza uzuri;kitu cha kupendezesha mahali Fulani.
Sisi tunakwenda kuzungumzia hiyo aina ya kwanza.

Baada ya kuyaona maneno haya,mpendwa tutambue kwamba katika ulimwengu wa Leo kuna aina nyingi sana za mapambo ambazo zinapamba na kupendezesha sshemu mbalimbali ya mazingira yetu,lakini pia yapo mapambo kwa ajili ya kuupendezesha mwili wa mwanadamu.

~Katika ujumbe huu napenda kuzungumza na nyie wanawake  mnaoipamba miili yenu kwa mavazi ya aibu ili ipendeze .
√ Sio kwamba wanaume hawavai vibaya Hapana ; bali leo Roho wa Bwana ameniongoza kusema nanyi akina mama.

Mimi binafsi nawatia moyo na kuwapongeza wanawake wote kwa habari kujipamba,nakuambia hivi jipambe sana tu ; lakini ni mapambo yapi ujipambe  ?  Fuatana nami.

~Katika dunia hii ya Leo najua kuna aina nyingi za saloon zenye hadhi mbalimbali na zina wataalamu wa viwango vya juu sana na wa tofauti tofauti;katika saloon hizo wanawake hutumia gharama nyingi sana ambazo zinawachukulia sehemu ya maisha yao.
~Saloon hizi zinabadirisha ngozi,shepu na hata miundo mbalimbali ya mapambo na wengine hujipamba hadi kupitiliza kiasi.Nakuambia wakina mama wanatumia gharama kubwa saba na wengine hata kugombana na waume zao pindi wakikosa kupewa hela ya kwenda saloon, wengine huenda mbali na kutafuta wanaume wa nje ya ndoa.

~Lakini nimegundua saloon moja,ambayo haitaji kuharibu pesa yako,wala kutafuta awara,wala kugharamikia kitu chochote kama unataka kupambwa.

    Sikiliza hii mpendwa 👂👂

👉 Siku moja nilikuwa napita mahali Fulani,nikaona akina mama Fulani wanaingia katika saloon moja hivi ya kifahari sana ili kwenda kujipamba wapendeze,mkononi mwangu nilikuwa na Saloon nzuri sana nakuambia we acha tu,saloon hii ikikupamba mpendwa kila mmoja atakupenda tu,utakuwa nuru gizani,utakuwa msaada wa walio wengi.
Na Saloon hii niliokuwa nayo si kitu kingine Bali nilikuwa na Biblia mkononi mwangu.

~Nilipowaona wale akina mama nikatamani niwashauri waje kwenye hii saloon niliyokuwa nayo ili wajipambe na wapambwe na wapendeze sana.Mpendwa nakuambia hivi Saloon hii haipo mbali na wala hauhitaji gharama nyingi bali gharama yako ni kuiamini na kuikubali biblia isemavyo.
~Basi nikaenda kuwaambia wale akina mama: Naomba mnisikilize kidogo,wakasema Hakuna shida mtumishi.
~Kwakuwa nilikuwa tayari nimejuwa wapi wanaenda na kufanya nini, nikawaambia Jamani Mimi ninayo Saloon nzuri sana hapa ambayo haihitaji gharama kama huko Mwendako.
~Wakasema Saloon hiyo iko wapi ili tusigharamikie?
Nikawaambia Saloon yangu ni BIBLIA hii tu.
~Wale akina mama walishtuka sana kusikia vile, walinishangaa sana ; nikawaambia msishituke naamini mtanielewa tu.

Niawaambia Hivi wewe mama Unakubalije kukaa bila kujipamba na wakati Biblia imekurusu?.
~Wakaniambia Kwanini umesema hivyo?

Nikawaambia tusome:
        1PETRO 3:5

√ Ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani,waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao√.

Wale akina mama washangaa,wakaniuliza mtumishi Wanawake wa zamani walijipambaje?

Nikawaambia na kuwajibu 👇

   Tusome 1PETRO 3:3-4

3 Kujipamba kwenu,kusiwe kujipamba kwa nje,yaani,kusuka nywele,na kutia dhahabu,na kuvaa mavazi;

4 Bali kuwe utu wa moyoni usioonekana,katika mapambo yasiyoharibika;Yaani,roho ya upole,na utulivu,iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.√

Hivyo nikawaambia enyi akina mama kwa mujibu wa Biblia kujipamba kwenu sio kwa nje Bali ni kwa ndani ya mioyo yenu.
Yaani muwe na roho ya utulivu,roho upole ndani yenu kwa mapambo haya hayaribiki kamwe.
~Wale akina mama wakaelewa,Uamuzi ukawa kwao kuifuata biblia au kuikataa;Mimi nikaondoka zangu.

Ewe mpendwa msikilizaji na msomaji wangu tunakiona na kugundua hapa ni kwamba:

~roho ya upole ni pambo.
~roho ya utulivu ni pambo.
Lakini pia mpendwa tujuwe kwamba:
~roho ya uvumilivu ni pambo.
~roho ya utu wema ni pambo.Na mengine mengi.

Mpendwa mapambo haya ni adimu sana kwa wanawake wa siku za Leo.Mapambo haya hayapatikani katika saloon yoyote ile hapa duniani,Bali yanapatikana Ndani ya Biblia tu.

✍ Ili ujuwe kuwa mtu ana roho ya utulivu ni pale yanapotokea machafuko na misukosuko.√
~Ukimuona mwanamke unatokea msukosuko kidogo  ndani yake,halafu anaenda kumtangaza mumewe nje ya ndoa yake, tambua ya kwamba huyo hajapambwa,hana ya uvumilivu na utulivu.
~Ili ujuwe mwanamke ana roho ya upole ndani Yake, ni pale inapotokea fujo, kelele,vurugu ndani ya ndoa yaani hapo utamtambua tu.
~Wanawake wengine wanakosa pambo la upole kiasi kwamba mumewe hatamani kurudi mapema nyumbani.

👉 Leo hii utakutana na mwanamke mkristo,lakini alivyojipamba sasa utaogopa kumwangalia Mara mbili;yaani inatia aibu jamani.
~Utamkuta amevaa kinguo kifupi sana,tena kimebana mwili wake, mapaja nusu utupu.
~Wengine wanavaa magauni mepesiiiii,wengine vitaiti na vipedo.
Ukimuangalia kichwani jamani ni hatari sana nakuambia, shedo utafikiri ameweka maji midomoni,wanja nayo, mmmmm....alafu hapo anasema biblia imeruhusu tujipambe.
~Na kanisani wanaingia,kukaa inakuwa shida,na watumishi tunakaa kimya tu.
Wengine mnatembea nusu uchi,nguo za ndani zikionekana,ramani ya.... Yote inaonekana.Jamani mnatutia aibu mjuwe.
~Ni kweli biblia imeruhusu ujipambe,lakini mapambo ya ndani yaani jipambe kwa roho ya upole,utulivu,uvumilivu,utu wema... Sio hayo mapambo ya mwili wako.

Wanawake jamani jipambeni kwa mapambo ya  ndani jamani,ni mapambo yasiyoharibika Bali yanadumu milele,hata ukinyeshewa na nvua hayatoki ndani yako. Jipambeni mwenendo safi na tabia njema ili muwavute maana hivyo ndivyo walivyojipamba wenzenu wa kale.

                👇👇

✍ Jipambeni Kwa roho ya Upole.

✍ Jipambeni kwa utu wema ndani ya mioyo yenu.

✍ Jipambeni kwa moyo wa utulivu.

✍ Jipambeni kwa mwenendo na  tabia njema .

✍ Jipambeni kwa adabu nzuri

Hujakatazwa kujipamba Ewe Binti yangu, ewe mama yangu Hujakatazwa kujipamba ; lakini jipambe kwa mambo tajwa hapo juu👆.
✅ Kwasababu mambo hayo hayaaribiki kamwe hata inyeshe Mvua kiasi gani.
-Ujisipambe kwa mavazi au Kwa dhahabu au Kwa lulu mwilini kwako ; bali Vaa mavazi ya Heshima, Mavazi ya Kuusitiri mwili wako.
✍ Achana Na hivyo vipedo, Vigauni Vifupi vyenye kuonyesha mapaja yako.

✍ Achana Na visiketi vifupi, Achana Na blouse zenye kuacha matiti yako nje nje jamani kwa maana hayo yanakudhalilisha ,yanaishusha thamani ya mwili wako, lakini pia yanaudharaulisha Wokovu wako ewe  Mama Na binti yangu katika Kristo.

√ Binti na  Mama yangu katika Kristo, Tunza thamani ya mwili wako ; heshimisha mwili. wako kila uendako ; huwezi kumuhubiria Mtu mmwingine Injili  ya Bwana Yesu Kristo Huku umevaa nusu uchi. √

No comments:

Post a Comment