Wednesday, January 31, 2018

MAISHA NA NENO LA MUNGU

MAISHA NA NENO LA MUNGU

Kanisa Bwana Yesu asifiwe

  Niseme kidogo Juu ya Huduma ya Kundi
Kundi hili La  kiroho Na Sio La kidini  Kazi Kuu Ni kuhakikisha Watu wanapata injili Na kubadilika Kwa Neno wanalolipata

Katika injili Kuna Huduma Kama Za kuwasaidia Yatima Na wajane Kama inavyosemeka Katika Yakobo 1:27

Agizo Kuu La YESU Kwa Kila anayempokea Ni kuhakikisha anamfikishia mwingine taarifa/Habari njema njema ili apate tumaini La kudumu

Marko 16:15-16

Mathayo 28:19-20

Pia zimezungumza Juu ya Jukumu hilo

Hivyo Basi Kundi linashughulika Na jambo La kupeleka injili Kwa Watu ili kuwatangazia Habari njema

Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Warumi 10:15

Kama Huu Mstari unavyosema Ndio sababu Ukiwa mmoja wa Watu ambao Tayari unayo nuru unaombwa Kutoa mchango wako ili injili ifike sehemu moja Na nyingine

Ni Utaratibu wa Kundi Kwa Kila mwakundi Kutoa sh.  17,000/= ikiwa Ni kiwango cha chini Na Pia unaweza Kutoa zaidi ya hapo

Endapo Kila mmoja Wetu Hapa atatoa kiasi hicho Basi tunaweza kufanya Mkutano mkubwa Sana

Unahimizwa Kutoa Maadamu Ni makubaliano ya Watu wa  Mahali hapa

Kiongozi wetu mkuu hakuona vyema Kundi liwe cha kuchati Tu Bali Watu wapone Kupitia Huduma Za humu ndani.

Zipo shuhuda nyingi ambazo Watu wamepona, wamebadilika

*Wahudumu wa Mkutano*

Watu wanaohudumu Ni wenyeji Yaani wale wa  Kanisa tutakaloshirikiana nalo pamoja wa Watu wa Mahali Hapa Hapa
[

Kwa sababu Hatuna Kanisa Kama Mahali Pa kukutania hivyo inatubidi tutafute Kanisa La kushirikiana nalo ili Watu watakaookoka wasibaki kutangatanga

Hivyo mtu wa Pwani Hakikisha ushirika wako unaonekana ili tuweze Kuvuna Mavuno Katika shamba La MUNGU

Wahubiri tunapenda Sana watoke Mahali Hapa Kwa sababu Mkutano tunauandaa Sisi hivyo Ni vyema ikiwa  tutasimama Pia Katika kuhudumu madhabahuni

Waimbaji Nafasi Ni zenu Hakikisha unajipanga ili kuhudumu Katika kile Ambacho Mungu amekiweka ndani yako
Tunao Wachungaji, Wainjilisti,  Manabii, n.k

Hivyo MUNGU Akupe Kibali ili Utumike.

Hatufanyi Mkutano Kwa Kutaka faida hivyo usiwazie sadaka zitakazotolewa Kwenye Mkutano

Vipo vitu vingi ambavyo vitafanywa Kupitia sadaka

Mwaka Huu utakuwa Ni Mkutano WA tatu

Mara ya kwanza Ulifanyika

Mkoani TABORA  Mwaka 2017

      June

Mara ya pili Dar es salaam ,June  2017

    Mara ya tatu  Ni Pwani 2018

Kuna mtu ameelewa Baadhi ya mambo kuhusu Mkutano Na Kundi
Sasa Basi Mungu akujalie Kutoa ili kuuwezesha Mkutano Na ukumbuke Kuwa Hatuna wafadhili WA Aina yeyote Ile ila Ni Mimi na Wewe  tuliopo  Mahali Hapa

Maombi yanahitajika Sana tena Sana ili Mungu atende Makuu Kupitia Huu mkutano

Mwaka Jana Mkutano ulifanikiwa Ni Baada  ya watakatifu WA Bwana kusimama Katika zamu Zao Na Kumsihi Mungu

Nina mambo Matatu ya kumalizia kwako wewe

1. Maombi Kwa ajili ya Mkutano Na Mungu aandae Watu Lakini Pia aende Nasi

2. Kujitoa kwako ili kufanikisha hili tulilolikusudia. Wewe ambaye YESU amesha kupa nuru yake jitahidi ufanye kitu Kwa ajili ya Bwana wa Majeshi

3. Mchango wako WA Pesa ili watakaofanikiwa kupata Kibali waende Na kufanya Huduma Hiyo Kama Mungu alivyokusudia

Wewe mwenye Huduma Na upo Mbali Na Eneo Husika wasiliana Na uongozi Mapema Sana ili Kama lipo La kuwezekana lifanyiwe kazi

Bila Pesa hatutafanya Mkutano Na Pesa zipo kwako hivyo utoe

Naomba Niishie Hapa
Kama una Swali Karibu

Bwana awalinde Siku Hii aonekane kwako wewe uliye dhaifu, akugange Wewe uliyevujika Moyo,  akuondoe Kwenye mateso yote, akupe amani Na furaha

   IMEANDALIWA NA
MWL ERICK MACHUMU

MAFIA - PWANI

KATIBU MKUU..
+255 752 763 020

©2018

MAISHA NA NENO LA MUNGU

Published by

ZAWADI NGAILO

SIKONGE TABORA

ADMIN MKUU
+255 762 450 772
©2018
MAISHA NA NENO LA MUNGU

What's up

https://chat.whatsapp.com/2yJswYBSEzLL8e7GaM6gq1

    

Saturday, January 27, 2018

ITAKIENI AMANI YERUSALEMU


  Mungu anatwambia tuiombea Amani Yerusalemu

Zaburi 122: 6 Utakieni Yerusalemu amani;Na wafanikiwe wakupendao;
7 Amani na ikae ndani ya kuta zako,Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zanguNiseme sasa, Amani ikae nawe.
9 Kwa ajili ya nyumba ya BWANA, Mungu wetu,Nikutafutie mema.

     Katika NENO hili tunaona kwamba kuomba Amani na mema kuja kwenye mji Mtakatifu ni FAIDA kwa wanaouombea ..

Mungu ameahidi  Baraka kwa wote wanaoitakia Baraka Israeli na laana wanao ilani.

Mwanzo 12:3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.

      Yerusalemu ni mji wa Wayahudi ,unafuatiwa na wale wanaouombea Amani na Ulinzi
Na Amani.

    Yerusalemu ni MAKAO ya Mungu  ya Amani.

Zaburi 125:5 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka,BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu.Amani ikae na Israeli

Yerusalemu ni mahali pa Kurudi kwa Yesu mara ya Pili

Zakaria 14:4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.

Matendo 1:11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Na Wakati Huo ataaanzisha Amani ya kudumu .
  Yesu anasema sisi tuwe watengenezaji wa Amani .
   Amani inatengenezwa kwa Kuombea Amani

Mathayo 5: 9 Heri wapatanishi;Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Pia tunatakiwa kuishi kwa Amani na watu wote .

   Warumi 12:18 Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.

Mungu anataka sisi kutafuta Amani na watu wote na tushiriki  katika maombi ya Amani  ndani ya Yerusalemu. Kwa kuwa ndio kiini cha moyo wake na MAKAO  yake.

Mungu akubariki

Wednesday, January 10, 2018

YESU NI MASIHI

   Yesu anaitwa Masihi Mathayo 1:16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
    Neno Kristo Lina maana ya Masihi .

Masihi ni Mpakwa mafuta

Agano la Kale lilitabiri habari za kuja kwa Masihi .

Na Agano jipya linatukumbusha kwamba Masihi ni Yesu Kristo .

Kuna mambo mengi ambayo wayahudi ( Watu wa uyahudi)
Walitarajia yatakuwa kwa Masihi kulingana na Ahadi iliyopo kwa Manabii wa Agano la Kale.

   Masihi atakuwa Mwebrania/Mwanaume wa Kiebrania

√ Isaya 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,Tumepewa mtoto mwanamume;Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;Naye ataitwa jina lake,Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,Baba wa milele, Mfalme wa amani.

√Atazaliwa Bethlehem Mica 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.

√Atazaliwa na Bikra  Isaya 7:14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.

Atakuwa nabii atakayetoka miongoni mwa ndugu
Kumbukumbu la Torati 18:18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.

√Atakuwa kuhani mfano wa Melkizedeki ( Melchizedek )

Zaburi 110:4 BWANA ameapa,Wala hataghairi,Ndiwe kuhani hata milele,Kwa mfano wa Melkizedeki.

√Atakuwa Mfalme

Isaya 11:1Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.
2 Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;
3 na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;
4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.

*Mwana wa Daudi

Mathayo 22:42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.

•Aliyeteseka kabla ya kuingia katika Utukufu wake
Isaya 53:1 Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta?Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani?
2 Maana alikua mbele zake kama mche mwororo,Na kama mzizi katika nchi kavu;Yeye hana umbo wala uzuri;Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu;Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko;Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu,Amejitwika huzuni zetu;Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,Alichubuliwa kwa maovu yetu;Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
6 Sisi sote kama kondoo tumepotea;Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe;Na BWANA ameweka juu yakeMaovu yetu sisi sote.
7 Alionewa, lakini alinyenyekea,Wala hakufunua kinywa chake;Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni,Na kama vile kondoo anyamazavyoMbele yao wakatao manyoya yake;Naam, hakufunua kinywa chake.
8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa;Na maisha yake ni nani atakayeisimulia?Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai;Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
9 Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya;Na pamoja na matajiri katika kufa kwake;Ingawa hakutenda jeuri,Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
10 Lakini BWANA aliridhika kumchubua;Amemhuzunisha;Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi,Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi,Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika.Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye hakiAtawafanya wengi kuwa wenye haki;Naye atayachukua maovu yao.
12 Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu,Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari;Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa,Akahesabiwa pamoja na hao wakosao.Walakini alichukua dhambi za watu wengi,Na kuwaombea wakosaji.

     Yesu Kristo alitimiza mahitaji yote /vigezo vyote vya Umasihi

Kwa sababu alikuwa ni wa kabila la Yuda

Luka 3:30 wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu,

√Alizaliwa Bethlehem  Luka 2:4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;
5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.
6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,
7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng?ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

√Alizaliwa na Bikra Luka 1: 26 Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.

   Ushahidi mwingine wa kwamba Yesu ni masihi alikuwa nabii kama Musa( Moses)..

Musa na Yesu wote ni manabii

Kumbukumbu la Torati 34:10 Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso;

Yesu Kristo ni nabii mkubwa kuliko Musa ...

Musa aliwatoa Israeli Utumwani lakini Yesu ametuokoa na kutuweka mbali hukumu ya Kifo na Dhambi .

Mbali na Musa Yesu Kristo hamwakilishi Mungu Bali ni Mungu  mwenyewe ..

Yohana Mtakatifu 10: 30 Mimi na Baba tu umoja.

Yesu Kristo hatuongozi tu kutufikisha Nchi ya Ahadi Bali anatuongoza sisi tufike Mbinguni na kuurithi Uzima wa Milele

√Yohana Mtakatifu  14:1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

Yesu Kristo ni nabii mkubwa kuliko Musa

Kama masihi alikuwa kuhani wa Kifalme ..

Hakuwa mlawi na mlawi tu ndio aliruhusiwa kuwa kuhani.

Yesu Kristo ni kuhani mfano wa Melkizedek

Mwanzo 14

Zaburi 110:4

Ni Mfalme wa Amani Waebrania 7:2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;

Yesu Kristo ni mkubwa kuliko Abraham

Yohana 8:58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.