MAISHA NA NENO LA MUNGU
Kanisa Bwana Yesu asifiwe
Niseme kidogo Juu ya Huduma ya Kundi
Kundi hili La kiroho Na Sio La kidini Kazi Kuu Ni kuhakikisha Watu wanapata injili Na kubadilika Kwa Neno wanalolipata
Katika injili Kuna Huduma Kama Za kuwasaidia Yatima Na wajane Kama inavyosemeka Katika Yakobo 1:27
Agizo Kuu La YESU Kwa Kila anayempokea Ni kuhakikisha anamfikishia mwingine taarifa/Habari njema njema ili apate tumaini La kudumu
Marko 16:15-16
Mathayo 28:19-20
Pia zimezungumza Juu ya Jukumu hilo
Hivyo Basi Kundi linashughulika Na jambo La kupeleka injili Kwa Watu ili kuwatangazia Habari njema
Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Warumi 10:15
Kama Huu Mstari unavyosema Ndio sababu Ukiwa mmoja wa Watu ambao Tayari unayo nuru unaombwa Kutoa mchango wako ili injili ifike sehemu moja Na nyingine
Ni Utaratibu wa Kundi Kwa Kila mwakundi Kutoa sh. 17,000/= ikiwa Ni kiwango cha chini Na Pia unaweza Kutoa zaidi ya hapo
Endapo Kila mmoja Wetu Hapa atatoa kiasi hicho Basi tunaweza kufanya Mkutano mkubwa Sana
Unahimizwa Kutoa Maadamu Ni makubaliano ya Watu wa Mahali hapa
Kiongozi wetu mkuu hakuona vyema Kundi liwe cha kuchati Tu Bali Watu wapone Kupitia Huduma Za humu ndani.
Zipo shuhuda nyingi ambazo Watu wamepona, wamebadilika
*Wahudumu wa Mkutano*
Watu wanaohudumu Ni wenyeji Yaani wale wa Kanisa tutakaloshirikiana nalo pamoja wa Watu wa Mahali Hapa Hapa
[
Kwa sababu Hatuna Kanisa Kama Mahali Pa kukutania hivyo inatubidi tutafute Kanisa La kushirikiana nalo ili Watu watakaookoka wasibaki kutangatanga
Hivyo mtu wa Pwani Hakikisha ushirika wako unaonekana ili tuweze Kuvuna Mavuno Katika shamba La MUNGU
Wahubiri tunapenda Sana watoke Mahali Hapa Kwa sababu Mkutano tunauandaa Sisi hivyo Ni vyema ikiwa tutasimama Pia Katika kuhudumu madhabahuni
Waimbaji Nafasi Ni zenu Hakikisha unajipanga ili kuhudumu Katika kile Ambacho Mungu amekiweka ndani yako
Tunao Wachungaji, Wainjilisti, Manabii, n.k
Hivyo MUNGU Akupe Kibali ili Utumike.
Hatufanyi Mkutano Kwa Kutaka faida hivyo usiwazie sadaka zitakazotolewa Kwenye Mkutano
Vipo vitu vingi ambavyo vitafanywa Kupitia sadaka
Mwaka Huu utakuwa Ni Mkutano WA tatu
Mara ya kwanza Ulifanyika
Mkoani TABORA Mwaka 2017
June
Mara ya pili Dar es salaam ,June 2017
Mara ya tatu Ni Pwani 2018
Kuna mtu ameelewa Baadhi ya mambo kuhusu Mkutano Na Kundi
Sasa Basi Mungu akujalie Kutoa ili kuuwezesha Mkutano Na ukumbuke Kuwa Hatuna wafadhili WA Aina yeyote Ile ila Ni Mimi na Wewe tuliopo Mahali Hapa
Maombi yanahitajika Sana tena Sana ili Mungu atende Makuu Kupitia Huu mkutano
Mwaka Jana Mkutano ulifanikiwa Ni Baada ya watakatifu WA Bwana kusimama Katika zamu Zao Na Kumsihi Mungu
Nina mambo Matatu ya kumalizia kwako wewe
1. Maombi Kwa ajili ya Mkutano Na Mungu aandae Watu Lakini Pia aende Nasi
2. Kujitoa kwako ili kufanikisha hili tulilolikusudia. Wewe ambaye YESU amesha kupa nuru yake jitahidi ufanye kitu Kwa ajili ya Bwana wa Majeshi
3. Mchango wako WA Pesa ili watakaofanikiwa kupata Kibali waende Na kufanya Huduma Hiyo Kama Mungu alivyokusudia
Wewe mwenye Huduma Na upo Mbali Na Eneo Husika wasiliana Na uongozi Mapema Sana ili Kama lipo La kuwezekana lifanyiwe kazi
Bila Pesa hatutafanya Mkutano Na Pesa zipo kwako hivyo utoe
Naomba Niishie Hapa
Kama una Swali Karibu
Bwana awalinde Siku Hii aonekane kwako wewe uliye dhaifu, akugange Wewe uliyevujika Moyo, akuondoe Kwenye mateso yote, akupe amani Na furaha
IMEANDALIWA NA
MWL ERICK MACHUMU
MAFIA - PWANI
KATIBU MKUU..
+255 752 763 020
©2018
MAISHA NA NENO LA MUNGU
Published by
ZAWADI NGAILO
SIKONGE TABORA
ADMIN MKUU
+255 762 450 772
©2018
MAISHA NA NENO LA MUNGU
What's up
https://chat.whatsapp.com/2yJswYBSEzLL8e7GaM6gq1
No comments:
Post a Comment