Mungu anatwambia tuiombea Amani Yerusalemu
Zaburi 122: 6 Utakieni Yerusalemu amani;Na wafanikiwe wakupendao;
7 Amani na ikae ndani ya kuta zako,Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zanguNiseme sasa, Amani ikae nawe.
9 Kwa ajili ya nyumba ya BWANA, Mungu wetu,Nikutafutie mema.
Katika NENO hili tunaona kwamba kuomba Amani na mema kuja kwenye mji Mtakatifu ni FAIDA kwa wanaouombea ..
Mungu ameahidi Baraka kwa wote wanaoitakia Baraka Israeli na laana wanao ilani.
Mwanzo 12:3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Yerusalemu ni mji wa Wayahudi ,unafuatiwa na wale wanaouombea Amani na Ulinzi
Na Amani.
Yerusalemu ni MAKAO ya Mungu ya Amani.
Zaburi 125:5 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka,BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu.Amani ikae na Israeli
Yerusalemu ni mahali pa Kurudi kwa Yesu mara ya Pili
Zakaria 14:4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.
Matendo 1:11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Na Wakati Huo ataaanzisha Amani ya kudumu .
Yesu anasema sisi tuwe watengenezaji wa Amani .
Amani inatengenezwa kwa Kuombea Amani
Mathayo 5: 9 Heri wapatanishi;Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Pia tunatakiwa kuishi kwa Amani na watu wote .
Warumi 12:18 Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
Mungu anataka sisi kutafuta Amani na watu wote na tushiriki katika maombi ya Amani ndani ya Yerusalemu. Kwa kuwa ndio kiini cha moyo wake na MAKAO yake.
Mungu akubariki
No comments:
Post a Comment