Yesu anaitwa Masihi Mathayo 1:16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
Neno Kristo Lina maana ya Masihi .
Masihi ni Mpakwa mafuta
Agano la Kale lilitabiri habari za kuja kwa Masihi .
Na Agano jipya linatukumbusha kwamba Masihi ni Yesu Kristo .
Kuna mambo mengi ambayo wayahudi ( Watu wa uyahudi)
Walitarajia yatakuwa kwa Masihi kulingana na Ahadi iliyopo kwa Manabii wa Agano la Kale.
Masihi atakuwa Mwebrania/Mwanaume wa Kiebrania
√ Isaya 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,Tumepewa mtoto mwanamume;Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;Naye ataitwa jina lake,Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,Baba wa milele, Mfalme wa amani.
√Atazaliwa Bethlehem Mica 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
√Atazaliwa na Bikra Isaya 7:14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Atakuwa nabii atakayetoka miongoni mwa ndugu
Kumbukumbu la Torati 18:18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
√Atakuwa kuhani mfano wa Melkizedeki ( Melchizedek )
Zaburi 110:4 BWANA ameapa,Wala hataghairi,Ndiwe kuhani hata milele,Kwa mfano wa Melkizedeki.
√Atakuwa Mfalme
Isaya 11:1Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.
2 Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;
3 na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;
4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
*Mwana wa Daudi
Mathayo 22:42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.
•Aliyeteseka kabla ya kuingia katika Utukufu wake
Isaya 53:1 Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta?Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani?
2 Maana alikua mbele zake kama mche mwororo,Na kama mzizi katika nchi kavu;Yeye hana umbo wala uzuri;Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu;Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko;Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu,Amejitwika huzuni zetu;Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,Alichubuliwa kwa maovu yetu;Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
6 Sisi sote kama kondoo tumepotea;Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe;Na BWANA ameweka juu yakeMaovu yetu sisi sote.
7 Alionewa, lakini alinyenyekea,Wala hakufunua kinywa chake;Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni,Na kama vile kondoo anyamazavyoMbele yao wakatao manyoya yake;Naam, hakufunua kinywa chake.
8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa;Na maisha yake ni nani atakayeisimulia?Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai;Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
9 Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya;Na pamoja na matajiri katika kufa kwake;Ingawa hakutenda jeuri,Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
10 Lakini BWANA aliridhika kumchubua;Amemhuzunisha;Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi,Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi,Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika.Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye hakiAtawafanya wengi kuwa wenye haki;Naye atayachukua maovu yao.
12 Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu,Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari;Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa,Akahesabiwa pamoja na hao wakosao.Walakini alichukua dhambi za watu wengi,Na kuwaombea wakosaji.
Yesu Kristo alitimiza mahitaji yote /vigezo vyote vya Umasihi
Kwa sababu alikuwa ni wa kabila la Yuda
Luka 3:30 wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu,
√Alizaliwa Bethlehem Luka 2:4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;
5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.
6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,
7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng?ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
√Alizaliwa na Bikra Luka 1: 26 Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
Ushahidi mwingine wa kwamba Yesu ni masihi alikuwa nabii kama Musa( Moses)..
Musa na Yesu wote ni manabii
Kumbukumbu la Torati 34:10 Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso;
Yesu Kristo ni nabii mkubwa kuliko Musa ...
Musa aliwatoa Israeli Utumwani lakini Yesu ametuokoa na kutuweka mbali hukumu ya Kifo na Dhambi .
Mbali na Musa Yesu Kristo hamwakilishi Mungu Bali ni Mungu mwenyewe ..
Yohana Mtakatifu 10: 30 Mimi na Baba tu umoja.
Yesu Kristo hatuongozi tu kutufikisha Nchi ya Ahadi Bali anatuongoza sisi tufike Mbinguni na kuurithi Uzima wa Milele
√Yohana Mtakatifu 14:1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Yesu Kristo ni nabii mkubwa kuliko Musa
Kama masihi alikuwa kuhani wa Kifalme ..
Hakuwa mlawi na mlawi tu ndio aliruhusiwa kuwa kuhani.
Yesu Kristo ni kuhani mfano wa Melkizedek
Mwanzo 14
Zaburi 110:4
Ni Mfalme wa Amani Waebrania 7:2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
Yesu Kristo ni mkubwa kuliko Abraham
Yohana 8:58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
No comments:
Post a Comment