U aminifu ni mojawapo
ya tunda la Roho
katika maandiko
matakatifu.
Tutajifunza uaminifu wa
Mungu unaopatikana katika
neno lake. Yeye amesema
atatimiza yale aliyoahidi katika
neno lake, si tu kwa wana wa
Israel bali kwa watu wote
wanaoishi sawasawa na neno
lake. Kwa hiyo, kwa upande
wetu inatupasa sisi nasi kuwa
waaminifu kwa kuliishi na
kulitenda neno la
Mungu. “Basi jueni ya kuwa
Bwana, Mungu wenu, ndiye
Mungu; Mungu mwaminifu,
ashikaye agano lake na
rehema zake kwao
wampendao, na kushika
amri zake, hata vizazi
elfu. Na itakuwa, kwa sababu
mwazisikiza hukumu hizi, na
kuzishika na kuzitenda, basi
Bwana, Mungu wako,
atakutimizia agano na
rehema aliyowaapia baba
zako.” Kum 7:9, 12. “Ndivyo
litakavyokuwa neno langu,
litokalo katika kinywa
changu halitanirudia bure
bali litatimiza mapenzi
yangu, nalo litafanikiwa
katika mambo yale
niliyolituma.” Isa 55:11.
Tabia ya mtu mwaminifu.
1. Mtu aliye mwaminifu ni yule
ambaye anatenda sawasawa na
maagizo, sheria na taratibu .
Ikiwa ni mtu aliyeajiriwa
katika kazi za nyumbani au ya
serikali anafanya kazi
ipasavyo, si mwizi, mpokea
rushwa, mdhulumaji na wala
si mwenye hila. Unaweza
kuona ilivyoandikwa kuhusu
mtumishi aliyeajiriwa kazi za
nyumbani ambaye alipaswa
kufanya kwa uaminifu. “Ni
nani basi yule mtumwa
mwaminifu mwenye akili,
ambaye bwana wake
alimweka juu ya nyumba
yake, awape watu chakula
kwa wakati wake? Heri
mtumwa yule, ambaye bwana
wake ajapo atamkuta
akifanya hivyo.” Mt 24:45-46.
2. Hatendi dhambi.Yusufu
mtumishi wa Potifa kwa kuwa
alikuwa mwaminifu
aliposhawishiwa na mke wa
Potifa ili kufanya naye dhambi
ya uzinzi alikataa. “....mke wa
bwana wake akamtamani
Yusufu, akamwambia, lala
nami. Lakini alikataa
akamwambia....Nifanyeje
ubaya huu mkubwa
nikamkose Mungu?” Mwa
39:7-9.
3. Hachukui kitu cha mtu
mwingine, iwe ni fedha, mali,
au kitu kingine chochote
ambacho si halali yake. Akitoa
fedha kwa ajili ya malipo
yoyote na akarudishiwa pesa
ya ziada hurudisha kiasi
kilichozidi. Ikiwa amemwona
mtu ambaye amedondosha
fedha au amepoteza kitu
chochote humrudishia. Kwa
kufanya hivyo analitii na
kulitenda neno la Mung
linavyosema, “Umwonapo
ng’ombe wa nduguyo au
kondoo wake
akipotea....sharti umrudishe
kwa nduguyo. Na kwamba
yule nduguyo hayuko karibu
nawe, na ukiwa humjui,
umchukue kwenu nyumbani
kwako, uwe naye hata aje
nduguyo kumtafuta, nawe
mrudishie....tena fanya vivyo
kwa kila kitu kilichopotea
cha nduguyo,....” Kum 22:1-3.
Umuhimu wa kuwa
mwaminifu.
Mkristo ambaye ameokoka
akiwa ni mwaminifu, Mungu
anamwamini na kumweka
katika kazi ya
utumishi. Tunaweza kujifunza
kwa baadhi ya watu ambao
Mungu aliwaona ni waaminifu
na kuwachagua na kuwafanya
kuwa watumishi wa kazi yake,
mfano wa Yesu, Musa
na Paulo “....Yesu aliyekuwa
mwaminifu kwake yeye
aliyemweka, kama Musa
naye alivyokuwa, katika
nyumba yote ya Mungu. Na
Musa kweli alikuwa
mwaminifu katika nyumba
yote ya Mungu
kama mtumishi....” Ebr
3:1,5. Mtume Paulo alikuwa ni
mwaminifu ndio
maana ameandika
akisema, “Namshukuru Kristo
Bwana wetu, aliyenitia nguvu
kwa sababu aliniona kuwa
mwaminifu, akaniweka
katika utumishi wake.” 1Tim
1:12.
Yampasayo mtu ili aweze
kudumu katika uaminifu.
Bwana wetu Yesu Kristo
alipokuwa hapa duniani kwa
sababu alikuwa ni mwaminifu
kila alipojaribiwa na
alizitambua hila za shetani
wala hakufanya kosa lolote.
Ndio maana ulipokaribia
wakati wa kukamatwa
aliwaambia wanafunzi wake
akisema, “....yuaja mkuu wa
ulimwengu huu hana kitu
kwangu.” Yn 14:30.
Kwa mkristo ambaye
ameokoka, amejazwa Roho
mtakatifu na kudumu katika
uaminifu, Roho mtakatifu
humfunulia hila zote za
Shetani anapojaribiwa.
Waliosimama imara katika
neno la Mungu Shetani huja na
kuwajaribu katika shida na
dhiki. Usikubali mawazo ya
shetani, bali mpinge na
kumkemea, kwa kumwambia,
nenda zako Shetani. “Ndipo
Yesu alipomwambia, Nenda
zako, Shetani,....Kisha Ibilisi
akamwacha....” Mt
4:10-11. “Basi mtiini Mungu.
Mpingeni Shetani, naye
atawakimbia, Mkaribieni
Mungu naye atawakaribia
ninyi....” Yak 4:7-8. Kutokana
na andiko hili mtu anaweza
kuwa karibu na Mungu na
kumkemea Shetani naye
huondoka, ikiwa analitii neno
na kuishi linavyosema.
Wale wote waliozaliwa mara
ya pili imewapasa kuushinda
ulimwengu na dhiki kwa
sababu aliye ndani yao ni
mkuu kuliko shetani, naye
Yesu alimshinda na
kushuhudia
akisema , “Ulimwenguni
mnayo dhiki; lakini jipeni
moyo; mimi nimeushinda
ulimwengu.” Yn 16:33 . Kwa
upande mwingine,
tunapolifahamu neno la Mungu
tunazitambua hila za shetani
na kumshinda. “Nao
wakamshinda kwa damu ya
mwana-kondoo, na kwa neno
la ushuhuda wao, ambao
hawakupenda maisha yao
hata kufa.” Ufu
12:11. “....Uwe mwaminifu
hata kufa, nami nitakupa taji
ya uzima....Yeye ashindaye
hatapatikana na madhara ya
mauti ya pili (Jehanum) .” Ufu
2:11-11.
Kinachotokea kwa mtu
anayedumu katika uaminifu.
1. Mungu humbariki na uzao
wake . “Mtu mwaminifu
atakuwa na Baraka tele” Mit
28:20.
“Mwenye haki aendaye
katika
unyofu (uaminifu) wake,
Watoto wake wabarikiwa
baada yake.” Mit 20:7.
2. Mungu anakuwa karibu
naye wakati anapomwita au
kumwomba. “Bwana yu
karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa
uaminifu.” Zab 145:18.
3. Anampendeza
Mungu. “Walio wakamilifu
katika njia zao
humpendeza.” Mit 11:20.
Monday, February 12, 2018
UAMINIFU
Sunday, February 11, 2018
SOMO :IMANI
MAANA YA IMANI
IMANI ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, Ni bayana ya mambo yasiyoonekana
Hiyo ni kwa mujibu wa Waebrania11:1
Katika maana hiyo ya imani tunazo sentensi mbili
Na ndani yake kuna maneno yanayobeba maana ya neno *imani*
Uhakika= ni ushahidi wa kutosha juu ya jambo tukio /fulani
Bayana= ni uwazi , dhahiri.Kwahiyo tunaposema hakika/uhakika maaa yake ni ushahidi wa kutosha
Mtu anapojaribu kuelezea tukio fulani watu huuliza, "una uhakika?"
Au wengine husema tutakuaminije?
Kwa maneno mengine Imani ni jicho la kuona vitu visivyoonekana
2wakorintho 5:7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)
Efeso 1:18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
Ndiyo maana katika warumi anasema
Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako na kuamini *moyoni* mwako..
Hapo utaona kuwa imani inakaa moyoni
Mwili wa mtu huwa gizani ikiwa macho yake ya moyo hayajatiwa nuru, na nuru hiyo ni
*Imani kwa kadiri imani ya mtu inavyoongezeka ndivyo anavyozidi kuona yuko katika nuru.
Ni kama vile nuru ya jua inavyoweza kufifia na kung'aa kwa nyakati tofauti tofauti
[2/11, 20:01] Masalu: *CHANZO* CHA *IMANI*
Warumi 10:17
Imani chanzo chake ni kusikia,
Na kusikia huja kwa neno la kristo
Kwa kadri mtu anavyozidi kusikia ndivyo imani yake huongezeka pia
Mtu akifuliza kusikia habari za uganga na uchawi imani yake hukuwa zaidi katika mambo hayo.
Ndiyo maana unakuta mtu anayeziamini habari za uganga si rahisi kumhamisha huko
Lakini imani yetu sisi hutokana na neno la kristo
Kwa kadri mtu anavyokuwa na bidii kusikia neno ndivyo imani yake pia hukua
Kwahiyo
Kiwango cha imani hutegemea kiwango cha Neno lililo ndani ya mtu.
Biblia inapozungumzia kusikia ni tofauti na kusikiliza au kujifunza peke yake, isipokuwa kulitunza Neno na kulitenda
Soma kumbukumbu 28: 1 Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
Kwa hiyo waweza jipima kwamba kiasi cha imani uliyo nayo ndiyo kiwango cha neno ulililo nalo.
Neno ni pumzi ya Mungu, hivyo kiwango cha imani yako ni kiwa cha Mungu ndani yako
*NGUZO* ZA *IMANI*
(MISINGI YA IMANI, MAWAKILI WA IMANI)
👆👆
Hivi ni vtu ambavyo vinasaidia utendaji kazi wa imani
Kama vile nyumba ili iwe imara inahitaji msingi lakini vilevile nguzo
1⃣UPENDO WA KI-MUNGU
Au nguvu ya uungu
1Yohana 4:7-8
7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
1 Yohana 4 :7
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
1 Yohana 4 :8
Mungu ni upendo
Hivyo basi ili mtu awe na Mungu ndani yake ni lazima awe na upendo
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Wagalatia 5 :6
Biblia inatuagiza katika wakorintho kwamba:
Kesheni simameni imara katika imani,...
Mambo yenu yote yatendeke katika upendo.
1 Wakorintho 16:13 Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.
14 Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.
👆👆
Hapo tunaona jinsi ambavyo neno imani linaambatana na upendo
Maana yake imani haiwezi kusimama peke yake pasipo upendo.
Katika hali ya kawaida ukipenda jambo fulani lazima una imani juu ya jambo hilo
Ukimpenda mtu vilevile utakuwa unamwamini
Lakini upendo ukiondoka huna imani naye tena hilo liko wazi
Hivyo msingi imara wa imani ni *UPENDO* tena wa ki-Mungu
Imani pasipo upendo haitendi kazi
1wakorintho 13: 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
Paulo anasema,
Hata angekuwa na imani kiasi gani lakini pasipo upendo ni sifuri au F
2⃣MATENDO
Hii ni nguzo nyingine ya imani
Yakobo 2:14, 22, 26
Kama vile mwili pasipo roho umekufa, kadhalika imani pasipo matendo nayo imekufa
Mtu anaposema ana imani lazima hiyo imani aiweke katika matendo lasivyo itakuwa ni imani mfu.
Tunahitaji kuona kile unachokiamini kinafanya kazi katika maisha yako
Hapo utaona yanatajwa mambo matatu,
Imani
Tumaini
Upendo
Lakini katika hayo yote lililo kuu ni upendo
*MAADUI* WA *IMANI*
1. HOFU NA MASHAKA
Mathayo 14:26-32
Mtu mmoja aniwekee mistari hiyo
Yakobo 1:5-6
1 Wakorintho 13:13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Mathayo 14:26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.
27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.
Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.
28 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
29 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.
30 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?
31 Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma.
32 Kilicho mfanya Petro aanze kuzama ni hofu
Maana aliamini kuwa ni Yesu ndiyo na akachukua hatua lakini imani yake ilishambuliwa na hofu
Yakobo 1:5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
Yesu akamshika mkono akamwambia
Ewe mwenye imani haba mbona uliona shaka?
Hapo utaona neno hofu na mashaka yalivyotumika kwa pamoja
Ndivyo ilivyo hata sasa kwamba mtu anaamini lakini dhoruba ikipiga imani inayumba kwa sababu ya kuruhusu hofu moyoni ambako ndiko imani inakaa
Mtu anapoomba
Na aombe kwa imani pasipo shaka yoyote
Kwahiyo palipo na shaka hapana imani, na kama imani ikiwepo kisha hofu akabisha hodi na kuingia basi imani huanza kuondoka taratibu
Waebrania 10:38
Yakobo1:5-6
5lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima,na aombe dua kwa Mungu,awapaye wrote,kwa ukarimu,wala hakemei;naye atapewa
6ila na aombe kwa imani pasipo shaka yo yote ;maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari liliochukuliwa name upepo na kupeperushwa huku na huku
Jambo jingine ni *kusitasita*
Hili nalo ni adui wa imani
Tena hapa Mungu anasema mwenye haki akisitasita roho yake haina furaha naye.
Kwa maana hiyo huwa tunapomhuzunisha Mungu pale tunapokuwa tumemwamini halafu bado tukaendelea kusitasita kwa kuona kwamba itakuwaje
Lakini kumbe kwake hakuna lisilowezekana
Mungu hututazama na kutuona vile tunahangaika huku tunasema tumemwamini anabaki anasikitika
Hapo ndipo inategemea unamjua Mungu kwa kiwango gani
Nimalizie kwa kukupa
*KAZI* ZA *IMANI*
1. Kuuona utukufu wa Mungu
Yohana 11:39-40
Utukufu-upako ama nguvu za Mungu
2. Kufuatwa na ishara
Marko 16:17-18
3. Kumshinda shetan 1Petro 5:7-8
4. Imani ni uhai wa mwili na roho.
Ebrania 10:38a
5. Imani huponya
Marko 5:34, 10:52
Kwa muda wako pitia maandiko hayo ili upate kujifunza,
Mungu wa mbinguni awabariki
@Mwalimu Samweli Masalu
Dodoma-Tanzania
Tuesday, February 6, 2018
Mombi
Maombi ni mawasiliano na Mungu
Ni mawasiliano na Muumba wetu ..
Mungu ni Roho
Yeremia 29:13 Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
Tunapomtafuta Mungu kwa Moyo wetu tunamuona
Biblia imejaa maongezi mengi /mazungumzo mengi kati ya Mungu na Watu wake tangu Bustani ya Eden.
Mwanzo 2: 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Mungu amemuumba Mwanadamu kwa ajili ya Ushirika pamoja na Mazungumzo yake.
Wakati Mungu anaongea na Adamu na Eva ilikuwa ni majibizano ya wazi.
Alizungumza nao na kuwapa maelekezo kwa njia ya Kawaida
Lakini kwa nyakati hizi njia ya kuwasiliana sisi na Mungu ni kupitia maombi
Maombi ni daraja LA kutuunganisha sisi pamoja naye
Zaburi 37 :4 Nawe utajifurahisha kwa BWANA,Naye atakupa haja za moyo wako.
23 Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA,Naye aipenda njia yake.
Maombi ni njia ya kutufanya sisi tufurahie uwepo wa Mungu katika MAISHA yetu
Ni njia ya kumfanya Bwana ajibu haja za mioyo yetu ..
Mioyo yetu imebeba mahitaji mengi hatuwezi kuyatua pasipo kutumia maombi
Maombi yanafanya hatua zetu ziimarishwe na Bwana .
Mungu mwenyewe ametualika sisi tumuite yeye na ameahidi kujibu au kutupa majibu ya kila tunachomuomba
Yeremia 3:3 Kwa sababu hiyo manyunyu yamezuiliwa, wala hapakuwa na mvua ya vuli; hata hivyo ulikuwa na kipaji cha uso cha kahaba, ulikataa kutahayarika.
Yeremia 29:12 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
Waefeso 6:18
Zaburi 50:15
1 Yohana 5:14
✍Unapomuita Mungu jua anaitika
Na unapokwenda kumuomba
Naye atakusikiliza
Yesu Kristo alitufundisha namna ya kuomba kupitia Sala yake kuu
Luka 11:2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]
3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].
Unapoomba Omba kwa Baba aliye Mbinguni
Jina lake litukuzwe
Ufalme wake uje nawe uishi humo
Mapenzi ya Mungu yatimizwe kwanza Kuliko yako
Pia akusamehe maovu na kukuepusha usiingie majaribuni
Pia rejea YOHANA Mtakatifu
Mlango wa 17 Hii inaonyesha Maombi ya karibu sana kati ya Mungu na Mwanae ( Yesu Kristo)
Ikiwa tumekuja kuwa wana wa Mungu kwa njia ya Imani katika Kristo tunaweza kuomba maombi ya karibu sana na kumjua Mungu wetu naye atatisikia .
YOHANA 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
Tunapokuwa karibu naye maana yake tunakuwa na Uwezo wa kufanya jambo lolote lile.
Miongoni mwa mifano itakayoonyesha jinsi Mungu anavyosema nasi na alivyoema na watu wengine .
✍Musa
Kutoka 4:10 Musa akamwambia BWANA Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.
✍Eliya Yakobo 5:17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
✍Daudi
2Samweli 24:10 Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu. Naye Daudi akamwambia BWANA, Nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa, Ee BWANA, nakusihi uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa.
✍Yesu
Mathayo 11:24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.
Yohana 17:1
Viongozi wakubwa watu wakubwa waliamini kuwa maombi ni njia ya kuwafikisha mahali pa juu zaidi.
Wana sayansi wakubwa pamoja na Ujuzi waliokuwa nao lakini
Waliamini nguvu ya Maombi
Mfano wao
Abraham Lincoln
Isaac Newton
Louis Pasteur
Francis Bacon
George Washington
Carver ,Galileo
HAWA pia waliamini katika Maombi na Sala .
Kila anayetembea karibu na Mungu wanaisikia sauti yake ,
Sauti ya Mungu ni ya Upole na inasema ndani ya Roho za Watu waliojitoa kweli kweli kwa Bwana .
Matendo 8:29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo.
Matendo 10:19 Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta.
2 Wakorintho 12:9
Anasema na watu wake kupitia Roho Mtakatifu
Anaishi ndani ya Roho na Mioyo ya watu waliokubali kujitoa kwake .
Anawaongoza
Anawalinda na
Kuwahamasisha katika kutenda yapendezayo machoni pake.
Warumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Wagalatia 5:18
Tunapoweka imani yetu kwa Yesu Kristo kwa ajili ya Ukombozi ...
Roho Mtakatifu anakuja kwetu na kuishi ndani yetu .
Anatusaidia sisi kuwasiliana na Mungu wetu kwa kuyatimiza mapenzi yake .
Mungu akubariki kwa ujumbe huu
By Zawadi Ngailo
Sikonge TABORA
What's up
+255 762 450 772