Sunday, February 11, 2018

SOMO :IMANI

MAANA YA  IMANI

IMANI ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, Ni bayana ya mambo yasiyoonekana
Hiyo ni kwa mujibu wa Waebrania11:1

Katika maana hiyo ya imani tunazo sentensi mbili

Na ndani yake kuna maneno yanayobeba maana ya neno *imani*

Uhakika= ni ushahidi wa kutosha juu ya jambo tukio /fulani

Bayana= ni uwazi , dhahiri.Kwahiyo tunaposema hakika/uhakika maaa yake ni ushahidi wa kutosha

Mtu anapojaribu kuelezea tukio fulani watu huuliza, "una uhakika?"

Au wengine husema tutakuaminije?

Kwa maneno mengine Imani ni jicho la kuona vitu visivyoonekana
2wakorintho 5:7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)

Efeso 1:18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;

Ndiyo maana katika warumi anasema

Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako na kuamini *moyoni* mwako..

Hapo utaona kuwa imani inakaa moyoni

Mwili wa mtu huwa gizani ikiwa macho yake ya moyo hayajatiwa nuru, na nuru hiyo ni
*Imani kwa kadiri imani ya mtu inavyoongezeka ndivyo anavyozidi kuona yuko katika nuru.

Ni kama vile nuru ya jua inavyoweza kufifia na kung'aa kwa nyakati tofauti tofauti
[2/11, 20:01] Masalu: *CHANZO*  CHA *IMANI*

Warumi 10:17

Imani chanzo chake ni kusikia,

Na kusikia huja kwa neno la kristo

Kwa kadri mtu anavyozidi kusikia ndivyo imani yake huongezeka pia

Mtu akifuliza kusikia habari za uganga na uchawi imani yake hukuwa zaidi katika mambo hayo.

Ndiyo maana unakuta mtu anayeziamini habari za uganga si rahisi kumhamisha huko

Lakini imani yetu sisi hutokana na neno la kristo

Kwa kadri mtu anavyokuwa na bidii kusikia neno ndivyo imani yake pia hukua

Kwahiyo

Kiwango cha imani hutegemea kiwango cha Neno lililo ndani ya mtu.

Biblia inapozungumzia kusikia ni tofauti na kusikiliza au kujifunza peke yake, isipokuwa kulitunza Neno na kulitenda
Soma kumbukumbu 28: 1 Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;

Kwa hiyo waweza jipima kwamba kiasi cha imani uliyo nayo ndiyo kiwango cha neno ulililo nalo.

Neno ni pumzi ya Mungu, hivyo kiwango cha imani yako ni kiwa cha Mungu ndani yako

*NGUZO* ZA *IMANI*

(MISINGI YA IMANI, MAWAKILI WA IMANI)

👆👆
Hivi ni vtu ambavyo vinasaidia  utendaji kazi wa imani

Kama vile nyumba ili iwe imara inahitaji msingi lakini vilevile nguzo

1⃣UPENDO WA KI-MUNGU
Au nguvu ya uungu

1Yohana 4:7-8

7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.

7  Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.

1 Yohana 4 :7

8  Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.

1 Yohana 4 :8

Mungu ni upendo
Hivyo basi ili mtu awe na Mungu ndani yake ni lazima awe na upendo

Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.

Wagalatia 5 :6

Biblia inatuagiza katika wakorintho kwamba:

Kesheni simameni imara katika imani,...

Mambo yenu yote yatendeke katika upendo.

1 Wakorintho 16:13  Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.

14  Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.

👆👆
Hapo tunaona jinsi ambavyo neno imani linaambatana na upendo

Maana yake imani haiwezi kusimama peke yake pasipo upendo.

Katika hali ya kawaida ukipenda jambo fulani lazima una imani juu ya jambo hilo

Ukimpenda mtu vilevile utakuwa unamwamini
Lakini upendo ukiondoka huna imani naye tena hilo liko wazi

Hivyo msingi imara wa imani ni *UPENDO* tena wa ki-Mungu
Imani pasipo upendo haitendi kazi
1wakorintho 13: 2  Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

Paulo anasema,

Hata angekuwa na imani kiasi gani lakini pasipo upendo ni sifuri au F

2⃣MATENDO

Hii ni nguzo nyingine ya imani
Yakobo 2:14, 22, 26

Kama vile mwili pasipo roho umekufa, kadhalika imani pasipo matendo nayo imekufa

Mtu anaposema ana imani lazima hiyo imani aiweke katika matendo lasivyo itakuwa ni imani mfu.

Tunahitaji kuona kile unachokiamini  kinafanya kazi katika maisha yako

Hapo utaona yanatajwa mambo matatu,

Imani

Tumaini

Upendo

Lakini katika hayo yote lililo kuu ni upendo

*MAADUI* WA *IMANI*

1. HOFU NA MASHAKA
Mathayo 14:26-32

Mtu mmoja aniwekee mistari hiyo

Yakobo 1:5-6
  1 Wakorintho 13:13  Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.

Mathayo 14:26  Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.
27  Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.
Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.

28 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

29 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

30 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

31 Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma.
32 Kilicho mfanya Petro aanze kuzama ni hofu
Maana aliamini kuwa ni Yesu ndiyo na akachukua hatua lakini imani yake ilishambuliwa na hofu

Yakobo 1:5  Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa

6  Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

Yesu akamshika mkono akamwambia

Ewe mwenye imani haba mbona uliona shaka?

Hapo utaona neno hofu na mashaka yalivyotumika kwa pamoja
Ndivyo ilivyo hata sasa kwamba mtu anaamini lakini dhoruba ikipiga imani inayumba kwa sababu ya kuruhusu hofu moyoni ambako ndiko imani inakaa

Mtu anapoomba

Na aombe kwa imani pasipo shaka yoyote

Kwahiyo palipo na shaka hapana imani, na kama imani ikiwepo kisha hofu akabisha hodi na kuingia basi imani huanza kuondoka taratibu

Waebrania 10:38

Yakobo1:5-6
5lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima,na aombe dua kwa Mungu,awapaye wrote,kwa ukarimu,wala hakemei;naye atapewa
6ila na aombe kwa imani pasipo shaka yo yote ;maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari liliochukuliwa name upepo na kupeperushwa huku na huku

Jambo jingine ni *kusitasita*
Hili nalo ni adui wa imani

Tena hapa Mungu anasema mwenye haki akisitasita roho yake haina furaha naye.

Kwa maana hiyo huwa tunapomhuzunisha Mungu pale tunapokuwa tumemwamini halafu bado tukaendelea kusitasita kwa kuona kwamba itakuwaje
Lakini kumbe kwake hakuna lisilowezekana

Mungu hututazama na kutuona vile tunahangaika huku tunasema tumemwamini anabaki anasikitika

Hapo ndipo inategemea unamjua Mungu kwa kiwango gani

Nimalizie kwa kukupa
 

*KAZI* ZA *IMANI*

1. Kuuona utukufu wa Mungu
Yohana 11:39-40
Utukufu-upako ama nguvu za Mungu
2.  Kufuatwa na ishara
Marko 16:17-18
3.  Kumshinda shetan 1Petro 5:7-8

4.    Imani ni uhai wa mwili na roho.
Ebrania 10:38a

5.   Imani huponya
Marko 5:34, 10:52

Kwa muda wako pitia maandiko hayo ili upate kujifunza,

Mungu wa mbinguni awabariki

@Mwalimu Samweli Masalu

Dodoma-Tanzania

1 comment: