U aminifu ni mojawapo
ya tunda la Roho
katika maandiko
matakatifu.
Tutajifunza uaminifu wa
Mungu unaopatikana katika
neno lake. Yeye amesema
atatimiza yale aliyoahidi katika
neno lake, si tu kwa wana wa
Israel bali kwa watu wote
wanaoishi sawasawa na neno
lake. Kwa hiyo, kwa upande
wetu inatupasa sisi nasi kuwa
waaminifu kwa kuliishi na
kulitenda neno la
Mungu. “Basi jueni ya kuwa
Bwana, Mungu wenu, ndiye
Mungu; Mungu mwaminifu,
ashikaye agano lake na
rehema zake kwao
wampendao, na kushika
amri zake, hata vizazi
elfu. Na itakuwa, kwa sababu
mwazisikiza hukumu hizi, na
kuzishika na kuzitenda, basi
Bwana, Mungu wako,
atakutimizia agano na
rehema aliyowaapia baba
zako.” Kum 7:9, 12. “Ndivyo
litakavyokuwa neno langu,
litokalo katika kinywa
changu halitanirudia bure
bali litatimiza mapenzi
yangu, nalo litafanikiwa
katika mambo yale
niliyolituma.” Isa 55:11.
Tabia ya mtu mwaminifu.
1. Mtu aliye mwaminifu ni yule
ambaye anatenda sawasawa na
maagizo, sheria na taratibu .
Ikiwa ni mtu aliyeajiriwa
katika kazi za nyumbani au ya
serikali anafanya kazi
ipasavyo, si mwizi, mpokea
rushwa, mdhulumaji na wala
si mwenye hila. Unaweza
kuona ilivyoandikwa kuhusu
mtumishi aliyeajiriwa kazi za
nyumbani ambaye alipaswa
kufanya kwa uaminifu. “Ni
nani basi yule mtumwa
mwaminifu mwenye akili,
ambaye bwana wake
alimweka juu ya nyumba
yake, awape watu chakula
kwa wakati wake? Heri
mtumwa yule, ambaye bwana
wake ajapo atamkuta
akifanya hivyo.” Mt 24:45-46.
2. Hatendi dhambi.Yusufu
mtumishi wa Potifa kwa kuwa
alikuwa mwaminifu
aliposhawishiwa na mke wa
Potifa ili kufanya naye dhambi
ya uzinzi alikataa. “....mke wa
bwana wake akamtamani
Yusufu, akamwambia, lala
nami. Lakini alikataa
akamwambia....Nifanyeje
ubaya huu mkubwa
nikamkose Mungu?” Mwa
39:7-9.
3. Hachukui kitu cha mtu
mwingine, iwe ni fedha, mali,
au kitu kingine chochote
ambacho si halali yake. Akitoa
fedha kwa ajili ya malipo
yoyote na akarudishiwa pesa
ya ziada hurudisha kiasi
kilichozidi. Ikiwa amemwona
mtu ambaye amedondosha
fedha au amepoteza kitu
chochote humrudishia. Kwa
kufanya hivyo analitii na
kulitenda neno la Mung
linavyosema, “Umwonapo
ng’ombe wa nduguyo au
kondoo wake
akipotea....sharti umrudishe
kwa nduguyo. Na kwamba
yule nduguyo hayuko karibu
nawe, na ukiwa humjui,
umchukue kwenu nyumbani
kwako, uwe naye hata aje
nduguyo kumtafuta, nawe
mrudishie....tena fanya vivyo
kwa kila kitu kilichopotea
cha nduguyo,....” Kum 22:1-3.
Umuhimu wa kuwa
mwaminifu.
Mkristo ambaye ameokoka
akiwa ni mwaminifu, Mungu
anamwamini na kumweka
katika kazi ya
utumishi. Tunaweza kujifunza
kwa baadhi ya watu ambao
Mungu aliwaona ni waaminifu
na kuwachagua na kuwafanya
kuwa watumishi wa kazi yake,
mfano wa Yesu, Musa
na Paulo “....Yesu aliyekuwa
mwaminifu kwake yeye
aliyemweka, kama Musa
naye alivyokuwa, katika
nyumba yote ya Mungu. Na
Musa kweli alikuwa
mwaminifu katika nyumba
yote ya Mungu
kama mtumishi....” Ebr
3:1,5. Mtume Paulo alikuwa ni
mwaminifu ndio
maana ameandika
akisema, “Namshukuru Kristo
Bwana wetu, aliyenitia nguvu
kwa sababu aliniona kuwa
mwaminifu, akaniweka
katika utumishi wake.” 1Tim
1:12.
Yampasayo mtu ili aweze
kudumu katika uaminifu.
Bwana wetu Yesu Kristo
alipokuwa hapa duniani kwa
sababu alikuwa ni mwaminifu
kila alipojaribiwa na
alizitambua hila za shetani
wala hakufanya kosa lolote.
Ndio maana ulipokaribia
wakati wa kukamatwa
aliwaambia wanafunzi wake
akisema, “....yuaja mkuu wa
ulimwengu huu hana kitu
kwangu.” Yn 14:30.
Kwa mkristo ambaye
ameokoka, amejazwa Roho
mtakatifu na kudumu katika
uaminifu, Roho mtakatifu
humfunulia hila zote za
Shetani anapojaribiwa.
Waliosimama imara katika
neno la Mungu Shetani huja na
kuwajaribu katika shida na
dhiki. Usikubali mawazo ya
shetani, bali mpinge na
kumkemea, kwa kumwambia,
nenda zako Shetani. “Ndipo
Yesu alipomwambia, Nenda
zako, Shetani,....Kisha Ibilisi
akamwacha....” Mt
4:10-11. “Basi mtiini Mungu.
Mpingeni Shetani, naye
atawakimbia, Mkaribieni
Mungu naye atawakaribia
ninyi....” Yak 4:7-8. Kutokana
na andiko hili mtu anaweza
kuwa karibu na Mungu na
kumkemea Shetani naye
huondoka, ikiwa analitii neno
na kuishi linavyosema.
Wale wote waliozaliwa mara
ya pili imewapasa kuushinda
ulimwengu na dhiki kwa
sababu aliye ndani yao ni
mkuu kuliko shetani, naye
Yesu alimshinda na
kushuhudia
akisema , “Ulimwenguni
mnayo dhiki; lakini jipeni
moyo; mimi nimeushinda
ulimwengu.” Yn 16:33 . Kwa
upande mwingine,
tunapolifahamu neno la Mungu
tunazitambua hila za shetani
na kumshinda. “Nao
wakamshinda kwa damu ya
mwana-kondoo, na kwa neno
la ushuhuda wao, ambao
hawakupenda maisha yao
hata kufa.” Ufu
12:11. “....Uwe mwaminifu
hata kufa, nami nitakupa taji
ya uzima....Yeye ashindaye
hatapatikana na madhara ya
mauti ya pili (Jehanum) .” Ufu
2:11-11.
Kinachotokea kwa mtu
anayedumu katika uaminifu.
1. Mungu humbariki na uzao
wake . “Mtu mwaminifu
atakuwa na Baraka tele” Mit
28:20.
“Mwenye haki aendaye
katika
unyofu (uaminifu) wake,
Watoto wake wabarikiwa
baada yake.” Mit 20:7.
2. Mungu anakuwa karibu
naye wakati anapomwita au
kumwomba. “Bwana yu
karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa
uaminifu.” Zab 145:18.
3. Anampendeza
Mungu. “Walio wakamilifu
katika njia zao
humpendeza.” Mit 11:20.
Monday, February 12, 2018
UAMINIFU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment