Saturday, February 4, 2017

MWANA WA ADAMU /MTU WA DUNIANI

      Bwana Yesu asifiwe!
Yesu Kristo alikuja duniani Kwa picha ya Mwanadamu halisi kusudi kuudhihirishia Ulimwengu kweli ya MUNGU  ..Lengo la kuja kwake kama Mwanadamu ilikuwa ni kuleta mamlaka ya MUNGU na Wanadamu Kwa pamoja

Biblia katika Zaburi 8:4 inasema "Mtu ni kitu gani hata Umkumbuke,Na binadamu hata umwangalie ?

       Tunapoyaangalia maisha yake tunatofautisha na Ya watu wengine Kwa sababu ya Upekee uliopo ndani yake ..
      Upekee wake unatokana na Kwamba ni yeye pekee aliyepaa Mbinguni  pia alishuka yeye pekee kutokabinguni

.YOHANA 3:13 inasema "Wala hakuna MTU aliyepaa Mbinguni ,ila yeye aliyeshuka kutoka Mbinguni ,Yaani Mwana Wa Adamu"

     Yohana 6:62 Itakuwaje basi Mmwonapo Mwana Wa Adamu akipaa huko alikokuwapo kwanza ?

       Yeye Kristo peke yake ndiye aliyeshuka toka Juu na ndiye anaweza kupandishwa juu tena ..

       Yesu Kristo akiwa na  Mungu na Wanadamu alileta mamlaka ya MUNGU katika Ulimwengu Wa Wanadamu ..

    Mamlaka iliyoletwa naye ni kusamehe Dhambi..

Marko 2:10  "Lakini mpate kujua Ya kwamba Mwana Wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi(hapo amwambia Wa kupooza.."
      Mwana Wa Adamu ni ndiye Bwana Wa sabato pia.. Mathayo 2:28

  MUNGU Kubariki sana

Na
ZAWADI NGAILO
P.o.box 124
Sikonge Tabora
©MAISHA NA NENO LA MUNGU

No comments:

Post a Comment