Tuesday, February 14, 2017

TUSIABUDU MIUNGU MINGINE

       Bwana Yesu asifiwe ..MUNGU wetu ametuumba kwa mfano na sura yake mwenyewe kusudi sisi tumtumikie yeye na kumuabudu yeye  wala si kitu chochote ..
      Kutoka 20:1 -2 MUNGU akanena maneno haya yote akasema  MIMI NI BWANA ,MUNGU WAKO ,NILIYEKUTOA KATIKA NCHI YA MISRI ,KATIKA NYUMBA YA UTUMWA ..

    Katika Mistari hii tunajifunza kwamba Mungu ni BWANA ,pia ni MUNGU wetu ..ambaye ametutoa Misri(Mahali penye mateso,Shida,Dhiki ) na kwenye Utumwa (kutumikisha na Dunia na wafalme wake).

             Wana WA Israeli walipokuwa misri waliishi maisha ya tabu sana na katika hali ya Utumwa ..Lakini MUNGU aliwapenda zaidi kisha akawatoa kutoka misri kwenda nchi ya Ahadi  (Kanaani )
  

    Lengo LA MUNGU kuwatoa eneo hilo halikuwa waache kumtambua na kumtumikia Yeye Bali ..wamtumikie Yeye mwenyewe .
            Ili kutokumwacha Mungu Lazima Tusiwe na miungu mingine Kutoka 20:3 inasema Usiwe na miungu mingine ila Mimi.
             Pia Tusifanye sanamu ya kuchonga au kitu chochote kilicho juu Mbinguni wala kilicho chini duniani,,wala kilicho majini chini ya Dunia..

           Watoto wa MUNGU tunapaswa kutokujiwekea Minara ama kusimamisha jiwe lolote katika Eneo lolote katika Nchi na kulisujudia Kwa kuwa yeye ni BWANA,MUNGU wetu ..

        ¶Tunapaswa Kuzishika Sabato za Bwana na kuheshimu madhabahu yake ..
Zaburi 81:10 inasema Mimi ndimi BWANA ,Mungu wako ,niliyekupandisha toka nchi ya Misri ;Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza "

   Tunapotambua kuwa Mungu ndiye MUNGU wa kweli ni vyema tuhakikishe vinywa Vyetu vinajaa Maneno yake na Pia tusikilize sauti yake kila  siku Asije akatuacha tuende njia mbaya Kwa sababu ya ukaidi wa Mioyo Yetu.

         Yeremia 25:6 MUNGU anasistiza kwamba Tusifuate miungu mingine ..ili kuitumikia wala tusimkasirishe Kwa kazi za mikono yetu na kujidhuru nafsi zetu ..

Mungu akubariki sana

No comments:

Post a Comment