Monday, March 13, 2017

FAIDA ZA KUMTEGEMEA MUNGU!, Hakuna aliyemtegemea Mungu akapata hasara, ukimtegemea Mungu kuna faida, hebu angalia hizi faida za kumtegemea Mungu:-  (1)Bwana atakupa haja ya moyo wako->ZABURI 37:4.  (2)Kila ulitendalo litafanikiwa->ZABURI 1:3, MITHALI 3:5-6.  (3)Utakuwa na Amani->AYUBU 22:21.   (4)Mema yatakuijilia->AYUBU 22:21.  (5)Utabarikiwa->YEREMIA 17:7, ZABURI 112:3.  (6)Uzao wako utakuwa hodari->ZABURI 112:2.  (7)Utamwona Mungu ktk maisha yako->YOHANA 14:21, MITHALI 8:17.   (8)Mungu anaweka ulinzi juu ya maisha yako->ZABURI 34:7, MITHALI 3:21-26.  (9)Bwana atasikia kilio chako yaani maombi yako->ZABURI 34:15.  Kumtegemea Mungu ndio Maisha ya ushindi kwa mkristo, 

No comments:

Post a Comment