.CHAGUA KUNYAMAZA
MITHALI 11:
12 Asiye na akili humdharau mwenziwe;Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
MITHALI 17:
28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima;Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba tunataka kuongea kila wakati, tunataka kujibu kila tunachokisikia, kila tunachokiona tunataka kukisemea kitu
Kuna wakati tunasikia na kukutana na mambo ambayo kiuhalisia moyo unagoma kabisa kunyamaza, unatamani ujibu, unatamani uwaambie watu yale umefanyiwa, unatamani uelezee vile umeumizwa lakini kumbe si kila jambo linatakiwa kuongelewa
Si kila ukionacho unatakiwa kukisemea kitu
Si kila usikiacho/uambiwacho ni lazima ujibu
Si kila ufanyiwacho ni lazima umwambie kila mtu
MUHUBIRI 3:
1 Kwa kila jambo kuna majira yake,Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona;Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
Ipo nguvu katika kunyamaza
Yapo mambo ambayo tunapaswa kuongea, kusema, lakini yapo mambo ambayo tunapaswa kunyamaza kwaajili ya usalama wa Roho zetu
Ni kweli kuna wakati unasemwa sana vibaya, unasingiziwa, unatukanwa nk nk, lkn ni lazima ukumbuke kwamba kuna mazingira ambayo hupaswi kujibizana hata kama umeumia kiasi gani
Unajua ni kwanini?
Ukisemwa vibaya, ukitukanwa, ukidharauliwa lazima moyo utaghafirika, moyo ukighafirika lazima utakuwa na hasira na ghadhabu
Ukiwa na hasira katu usitegemee kuwa utajadiliana na mtu kwa hekima
Ukiongea utaongea katika uwepo wa hasira, ukijibu utajibu kulingana na kiwango cha hasira ulichonacho.
"AKUSHINDAE KUONGEA, MSHINDE KUNYAMAZA".....
No comments:
Post a Comment