Wednesday, March 8, 2017

NGUZO YA SIKU

Zaburi 24:1
. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.

Zaburi 24:2
. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.

Zaburi 24:3
. Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?

Zaburi 24:4
. Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.

Zaburi 24:5
. Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.

Zaburi 24:6
. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

Zaburi 24:7
. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.

Zaburi 24:8
. Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita.

Zaburi 24:9
. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.

Zaburi 24:10
. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu. Kama TU MALI YA BWANA NA MALI, ELIMU NA CHOCHOTE ALICHONACHO MTU NI MALI YA BWANA, KWA SABABU HIYO BASI IMETUPASA KUWA TAYARI KUKABIDHI MIOYO YETU AITAWALE YESU, Niwatakie asubuhi njema

No comments:

Post a Comment