Sunday, September 10, 2017

UKOMBOZI


1 Yohana 1:7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

Tunapoenenda katika nuru tunashirikiana na Kristo
Palipo na nuru Macho huo vizuri ..Ukitembea Nuruni huwezi kujikwaaa

a) Damu ya Kristo ni Upatanisho

Damu inapatanisha ..Tumetenganishwa na Dhambi lakini Damu ya Yesu imetupatanisha na Mungu /,kutoka katika dhambi.

Wakosai 1:20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.

       Kwa Damu ya Yesu tumekombolewa ..
       
Damu lazima isafishe dhambi zote..

Ufunuo 7:13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?
14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya.

     Kanisa lazima Liwe Takatifu ..

Aliyeshinda dhambi ndio mshindi wa kuingia Mbinguni ..

Damu ya Yesu imekuja kututengeneza ..

Damu ya Yesu ipo kwa ajili ya Mtenda dhambi

Ipo kwa ajili ya MAISHA yetu.

Unapoaasi dhbi inakupata ..

Ni wakati wa kuutazama Msalaba  wa Yesu ..

Bila kuwagiwa kwa Damu Kristo tiungeangamia

Waebrania : Mlango 13

12 Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango.

       Damu ni upatanisho wa nafasi zetu na Mungu..

Walawi 17 :11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.

Tunamshinda Shetani kwa njia ya Damu ya Yesu Kristo peke yake.
    
Ufunuo 12:
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.

Friday, September 8, 2017

MADHABAHU

MADHABAHU ni mahali rasmi ambapo watu au mtu hutumia kufanya ibada kwa Mungu au mungu ambaye ndiye mwabudiwa. Kuna utofauti kati ya mungu wa herufi ndongo na Mungu huyu wa herufi kubwa ya mwanzo , huyu ni mungu wa dunia hii ambaye hakuumba mbingu na nchi ,ila Mungu wa herufi kubwa ya mwanzo huyu ndiye Mungu muumbaji.
Kutoka 20:2-3 ‘‘Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miung mingine ila mimi. ”
MUHIMU: usitumie herufi ndogo mwanzoni unapo andika kumwakilisha Mungu wa muumbaji, ni kosa kubwa sana.
IBADA HUJUMUISHA YAFUATAYO; Kuadhimisha, kutoa sifa , kutoa sadaka ,kuomba na kumtumikia Mungu au mungu.
Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani , na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israel, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyo andikwa katika toati ya Musa , mtu wa Mungu. Ezra 3:2
AINA ZA MADHABA
(i) Madhabahu ya Mungu wa mbinguni.
Je Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu.Yakobo 2:21.
Hii ni madhabahu ya kweli ambayo ndiyo iliyo sahii kwa mtu aliye mwamini Yesu kuijua kwa undani zaidi.
(ii) Madhabahu za kishetani. Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene , katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari mambo ya dini. Kwasababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya Ibada yenu, naliona madhabahu iliyo andikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYE JULIKANA. Basi mimi nawahubiri habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Matendo 17:22-23.
Ni dhahiri kwamba mtume paul aliyo iyona ni madhabahu ya kishetani ambayo ipo kinyume na mapenzi ya Mungu wa Kweli. Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.1korintho10:14-22. Ibada ya sanamu ni ipi? ni ibada inayo fanywa kwa mungu wa dunia hii, ambaye ni shetani.
HIZI NI BAADHI YA MADHABAHU ZA KISHETANI.
(a) Madhabahu za maji. Unaweza kuwa shahidi katika jambo hili yapo baadhi ya makabila ndani ya Nchi hii ya Tanzania na nchi nyingi duniani. Ambao hufanyia baadhi ya Ibada kwenye mito, baharini, maziwa na mabwawa katika maeneo haya watu huenda kutoa sadaka, au huita kutambika. Tambua maji yanasikia kwahiyo upo uhusiano mkubwa katika ulimwengu wa roho kati ya maneno yanayo tamkwa kipindi cha kutoa sadaka. Tusome 2wafalme 2:19-22 Watu wa mji wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama Bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. Akaseme,Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.
(b) Misitu na miti mikubwa. hii pia hutumika kama maeneo ya kufanyia Ibada za kishetani ambazo huusisha utoaji wa sadaka.
(c) Njia panda. Hili si geni kwa watu wengi katika miji na vijiji pia limekuwa likifanywa , kwa kutumia njia panda kama sehemu ya kutoa sadaka mbalimbali mfano; Nazi kuvunjwa, vibuyu kuvunjwa.
(d) Nguzo maalumu na minara. Haya yote yamekuwa maeneo ya kutolea sadaka katika miji mikubwa ambayo hasa vizazi na vizazi hulithi utamaduni huu.
(e) Milima. hasa milima mirefu hutumika kama maeneo muhimu katika Ibada za kishetani, na tambua kwamba tunapo ongelea ibada, Hakuna ibada pasipo kutoa sadaka. Swali ni kwamba sadaka hiyo inatolewa kwa nani ?
(f) Madhabahu za mateso.
Hizi humilikiwa na watu mfano, Wachawi, Waganga, Wanajimu na makuhani wa sanamu, hawa wote wanakuwa na kibali cha kipepo katika kuendesha ibada hizo ila kwa lengo la kutesa maisha ya watu tu.
Kazi yao ni kutengeneza Madhabahu hizo kwa ajili ya kupeleka Nguo, Majina, Picha,Vitu ,Fedha na visanamu vya watu wanaotaka wawatese. sababu hii hupelekea watumishi wa Mungu kuwafundisha sana, wakristo kuwa makini katika maisha yako ya kila siku ,una kula nini? Una vaa nini? Una ongea nini? yote haya katika ulimwengu wa roho yana umuhimu na yanaweza kumuonganisha mkristo hata yeye pasipo kujua.
Pamoja na kuangalia mfumo wa madhabahu za kishetani iko nguvu zaidi kwa madhabahu ya Mungu wa mbinguni. Mfano Elia na manabii. 1Wafalme 18:30-35, Jitahidi sana kuisoma habari hii yote na utaona jinsi ambavyo madhabahu ya ki-Mungu ilivyo na nguvu , ambazo ziliweza kumdhihirisha kuwa yeye ni Mungu mkuu.
MUHIMU: pasipo madhabahu hakuna msingi imara wa kiroho.
FAHAMU HATUA ZA KUJENGA MADHABAHU.
Jambo la kwanza fahamu ,Madhabahu zote za ki-Mungu lazima ziungamanishwe na kanisa lililopo hapa duniani.
Madhabahu yaweza kuwa ya mtu mmoja au kikundi cha watu wengi.
Mfano, Agano la kale Ezra 3:5 walitumia hasa kuchinja wanyama , ila kwa Agano jipya utaratibu hasa sa ni sadaka pasipo damu ya wanyama. Ila unaweza toa ; Pesa ,mnyama au kitu chochote
FAIDA YA MADHABAHU YA KI- MUNGU
(i) Huweka upatanisho (msingi)
Madhabahu ya ki-Mungu pale mwamini anapotoa sadaka, jambo la kwanza ni “UPATANISHO”
Mwanzo 18:6-10 ili Upatanisho uwe dhahiri ni endapo tu kutoa kutakuwa kwa moyo wa kupenda. Mfano unapo soma maandiko hayo yanaonyesha Baba wa Imani akifanya kwa kupenda na si kulazimiswa na watu, Ibrahimu alijua siri.
Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia , Ee Ibrahimu, Naye akasema , Mimi hapa. Akasema, umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye , Isaka , ukaende zako mpaka nchi ya moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu yam mlima mmojawapo nitakaokuambia. Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa. Mwanzo 22:1-3.
Kiukweli si kwamba Ibrahimu jambo hili katika hali ya kibinadamu lilikuwa lahisi kwake, ila mtumishi wa MUNGU huyu alijua maana ya madhabahu, Madhabahu unapo jenga huanzia rohoni kwanza kwahiyo pale alipo kubali kumtoa Isaka Kuwa sadaka ya kuteketezwa tayari alikuwa amejenga.
MUHIMU: Kwa kila jimbo, ulifanyalo kuwa makini katika kujenga Madhabahu.
(ii) Hufungulia Baraka.
Kupitia Madhabahu ya Mungu wa Israel, inaleta baraka za haki isivyo kawaida.
Ukisoma, Mwanzo 22:15-18 ''Malaika wa BWANA akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni. akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.''
Katika maisha yako ya kawaida jitahidi kabla ya kuomba Baraka, fanya kitu kwanza mbele za Mungu.
Soma maneno haya pia utaona jinsi Mungu anavyo toa maagizo kwa balaamu kuwa akanene na Baraki.Hesabu 23:16-20
Jitahidi upitie vifungu hivi pia vitakavyo kujenga sana juu ya baraka za KiMungu.
''na Baraka hizi zote zitakujulia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani'' Kumb 28; 2, 8.
''Atawabarikia wamchao BWANA, Wadogo kwa wa kubwa.'' zaburi 115:13
Atukuzwe Mungu , Baba wa Bwana wetu Yesu kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni , katika ulimwengu wa roho, ndani yake kristo. Efe 1:3
MUHIMU: tambua mambo ya rohoni huzaa na baadaye huja ya kimwili. Galatia 3:9 Unapofanya jambo hili Imani huitajika sana.
Tulio mwamini Yesu, wote tumebarikiwa ili kuzifanya Baraka ziwe dhahiri maishani mwako LAZIMA UFANYE KITU. Matendo ya mitume 3:25-26. ''Ninyi mmekuwa watoto wa Manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na Baba zenu, akimwambia Ibrahimu, katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.''
(iii) Ulinzi wa Ki-Mungu.

Tambua Mungu wetu ni Mungu wa Maagano huachilia ulinzi katika maisha ya mtu kwasababu pale anapo mtazama mtu huyo huona “AGANO”. Mfano, ukisoma mandiko haya yote yanazidi kuonyesha faida ya maagano. Nuhu, Mwanzo 6:18, 9:11. ''Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe na wanao, na mkeo na wake za wanao, pamoja nawe. na agano langu nitalithibitisha nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika , baada ya hayo, kuiharibu nchi.''
Maandiko yote haya yanaonyesha kuwa kupitia sadaka huweka agano ambalo Mungu huliangalia hilo kwa kipindi kirefu sana.
Ibrahimu, Mwanzo 17:4 ''mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi.'' Mungu wetu ni Mungu wa Maagano yeye huweka na hilo agano hudumu kwa kipindi kirefu sana, unapo toa sadaka inakuwa agano mbele za Mungu ambalo hudumu kwa kipindi kirefu sana.
Kumb 29:25 ‘‘Ndipo watakaposema watu, ni kwa kuwa waliacha agano la BWANA, Mungu wa baba zao, alilofanya nao hapo alipowatoa katika nchi ya Misri’’.
(iv) Humkumbusha Mungu. Jambo hili ni siri kubwa sana, Madhabahu huongea yaani Inasema mbele za Mungu. Zaburi 106:45 ''Akawakumbukia agano lake ; Akawahurumia kwa wingi wa fadhiri zake.''
Ufunuo 16:7a.''Nikasikia hiyo madhabah ikisema'' Kwahiyo katika maisha ukiwa kama mwamini unapo kuwa na tabia ya kujenga madhabahu kwa mambo uyafanyayo ,kwasababu kutokana na shughuri mbalimbali za kimaisha upo wakati utasahau wewe binafsi kama ulifanya kitu mbele za Mungu, ila Hiyo Madhabahu “ITASEMA MBELE ZA MUNGU KWAAJILI YAKO”
(V) Humdhiirisha Mungu au humfunua. 1wafalme 18:22, 32-38 ukisoma vizuri na kwa umakini utagundua kuwa ugomvi au ubishani uliokuwepo kati ya nabii Eliya na Manabii wa Baali ulikuwa nani Mungu wa kweli kati ya Mungu wa Eliya na wao Baali, ubishano wao ulikuwa mkubwa sana ambao usingwezwa kuisha kwa uhalaka kwasababu IMANI ni kitu cha thamani kwa mtu aliye nacho ,pale anapo amini juu ya jambo fulani si kwa ulahisi unaweza mwambia usiamini, ni mpaka pale UDHIHIRISHO unapo tokea. Kwahiyo Nabii Eliya akawaambia ‘‘kwa hiyo na watutolee ng’ombe wawili; wao na wajichagulie ng’ombe mmoja, wamkate-kate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza ng’ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni,wala sitatia moto chini. Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la bwana; na Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu”.
Kiukweli katika maneno hayo, kinacho tamkwa ni kwamba LEO NA TUONE NANI ALIYE WA KWELI KATI YA mungu au MUNGU.
KITU CHA KUFANYA
Kama hukuwahi kujenga madhabahu jitahidi kujitoa kwanza kwa kujengea vitu vyako vyote ukianzia ,watoto wako, ndugu kiujumla. elimu ,biashara ili uviungamanishe na Mungu, pia baada ya kuyajua yote haya ,JITAHIDI UYAFANYIE KAZI NA MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI.

Wednesday, September 6, 2017

KUBEBEANA MIZIGO

.          ”Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri Zake.”_ (Danieli 9:3, 4).*

Akiwa na mzigo kwa niaba ya Israeli, Danieli alijifunza upya unabii wa Yeremia. Ulikuwa waziwazi kiasi ambacho kwenye vitabu alielewa shuhuda hizi zilizorekodiwa “hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.”

Kwa imani ambayo msingi wake ulikuwa kwenye neno la unabii lililo imara zaidi, Danieli alimsihi Bwana kwa ajili ya kutimizwa upesi kwa unabii huu. Alisihi kwa ajili ya heshima ya Mungu kudumishwa. Katika ombi lake alijiweka yeye mwenyewe kikamilifu pamoja na wale waliokuwa wamepungua katika makusudi ya Mungu, akiungama dhambi zao kana kwamba ni zake mwenyewe.

Ombi lililotoka kwenye midomo ya Danieli lilikuwa la ajabu sana! Linadhihirisha nafsi iliyonyenyekea kiasi cha ajabu! Joto la moto wa kimbingu lilitambulika katika maneno yaliyokuwa yakipanda juu kwa Mungu. Mbingu ilijibu ombi lile kwa kumtuma mjumbe wake kwa Danieli. Katika siku zetu hizi, sala zinazowasilishwa namna hiyo zitashinda pamoja na Mungu. “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana.”

Kama ilivyokuwa nyakati za kale, ombi lilipotolewa, moto ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza kafara iliyokuwa juu ya madhabahu; hivyo, kama majibu kwa ajili ya maombi yetu, moto wa kimbingu utakuja kwenye roho zetu. Nuru na uwezo wa Roho Mtakatifu vitakuwa vyetu. Je, sisi hatuna hitaji kubwa la kumwita Mungu kama alivyokuwa Danieli? Ninanena na wale wanaoamini kwamba tunaishi kwenye kipindi cha mwisho kabisa cha historia ya dunia hii. Ninawasihi mbebe mioyoni mwenu mzigo kwa ajili ya makanisa yetu, shule zetu na taasisi zetu.

Mungu yule aliyesikia maombi ya Danieli atasikia maombi yetu tunapomjia kwa moyo wa toba. Mahitaji yetu ni ya muhimu pia, matatizo yetu ni makubwa na tunahitaji kuwa na makusudi yenye mkazo uleule, na kwa imani tumtwike mzigo wetu yeye aliye Mbeba-mizigo mkuu. Lipo hitaji kwa ajili ya mioyo kuguswa sana wakati wetu kama ilivyokuwa wakati Danieli alipoomba.

Tuesday, September 5, 2017

FAHARI YA KIJANA NI NGUVU ZAKO

Bwana Yesu Kristo atukuzwe wana wa Mungu aliye hai.
Ninazidi kumshuru Mungu kwa ulinzi wake na kuzidi kutukutanisha tena, jina la Bwana lihimidiwe.

Karibu sana mpendwa tusemezane katika ujumbe huu wa neno la Mungu ambao Roho wa Mungu ametupatia.

Ujumbe:FAHARI YA KIJANA NI NGUVU ZAKO.
               ======================

Katiika ujumbe wetu naomba kuzungumza na kusemezana na vijana wote wa kike na wa kiume,na labda Roho wa Mungu atasema nawe hata kama sio kijana basi naomba ulipokee neno hilo litakusaidia.

         Tusome MITHALI 20:29

Fahari ya kijana ni nguvu zao;Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.

Nguvu
---------- Ni uwezo unaomsababisha mtu kufanya jambo Fulani katika maisha yake.

➡Hizo nguvu ambazo unazo wewe kijana,naomba nikuambie kwamba Mungu hajakupa nguvu hizo kwa ajili ya:
👉Kuiba,kubaka,kubomoa nyumba za watu,wala hujapewa nguvu hizo kwa ajili ya kupiga watu,wala sio za kutukana wazee mitaani.

👉Bali  Mungu amekupa nguvu hizo kwa ajili ya kumtumikia,kwa ajili ya kufanya kazi nzuri za mikono yako naye akubariki,kwa ajili ya kuwasaidia wengine mpendwa.
➡Hivyo Tumia nguvu ulizonazo leo kumtumikia Mungu wako kijana wangu.

👉Lakini vijana wengi Leo tunazitumia hizo nguvu zetu vibaya sana nakuambia mpendwa; wengine wanazitumia kuvuta madawa ya kulevya,wengine kuiba,wengine kubaka mitaani,wengine kupigana,wengine kutukana watu.

➡Nakuambia wewe kijana utumiaye nguvu zako vibaya wakati wa ujana wako,nakuambia siku inakuja ambayo utazitafuta nguvu hizo.
➡Wengine husema siwezi kumtumikia Mungu nikiwa kijana,Bali nitamtumikia Mungu nikiwa mzee,hivi calender ya maisha yako unayo wewe mikononi mwako?.

      Soma hii hapa MHUBIRI 12:1-2

1⃣Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako,Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,Wala haijakaribia miaka utakaposema,Mimi sina furaha katika hiyo.

2⃣Kabla jua,Na nuru na mwezi,na Nyota havijatiwa Giza;Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;....

👉Unaona hapo 👆wewe kijana mwenzangu;neno linakuambia tumkumbuke Muumba wetu ambaye ni Mungu wetu katika siku za ujana wetu,kumbuka  kumtumikia BWANA Eee kijana .
➡Nakushangaa wewe unayesema kwamba unasubiri uwe mzee ndio utamtumikia Mungu.

👉Siku zinakuja wewe kijana ambazo hizo nguvu zako unazoziaribu Leo utazitafuta nakuambia.
➡Mungu anataka tumtumikie Maishani mwetu tukiwa bado tuna nguvu wapendwa.
➡Usisubiri umekuwa mgonjwa ndio sasa unakumbuka Mungu yupo,jitambue bado usiku haujakufikia mpendwa.

👉Acha kutumia nguvu zako kuwatukana wazee nakuambia kijana mwenzangu.Wewe ujajivunia huo ujana wako na kuanza kuwadharua na kuwatukana wazee,nakuambia huyo mzee unayemtukana na kumdharau alikuwa kijana kama wewe.

👉Yaani kinywa chako kimejaa matusi,maneno machafu dhidi ya wazee,nakuambia ole kwako.
➡Unajivunia nguvu zako kwa kuvuta bangi,naomba nikuambie kwamba hata na huyo mzee nguvu alikuwa nazo.

Wahenga walisema kwamba:
➡Kuishi kwingi ni kuona mengi√.
Sasa wewe huyo mzee unayemdharau alishayaona mengi sana,je utaomba ushauri kwake? Muheshimu mzee mpendwa kijana.

➡Tambua kwamba Wewe sio wa kwanza kuwa kijana,wapo waliokutangulia wewe ambao waliwaheshimu wazee wao na maisha yao yakawa mazuri sana,na Mungu akawafanikisha na kuwainua zaidi.

      Ona vijana hawa:

👉Kijana Yoshua alimuheshimu sana Musa,na baada ya kifo cha Musa Mungu akamuinua Yeye.

👉Kijana Samweli alimuheshimu sana Eli na akawa kijiana mwenye maadili mema,na Mungu akamtumia zaidi.

👉Kijana Timotheo alimuheshimu Paulo.
Na wengine wengi mpendwa ambao waliwaheshimu wazee wao;waliyasikiliza mausi,ushauri na maonyo yao, na Mungu akawainua zaidi na zaidi;kwanini wewe unamdharau mzee huyo?

👉Ni kweli kwamba Mungu ameiweka huduma kubwa ndani yako,lakini tambua unahitaji ushauri wa wazee ili uzidi kusonga mbele zaidi;acha kuwadharau na kuwatukana ewe kijana mwenzangu.

Jambo la kusikitisha ni kwamba:

➡Vijana wengi makanisani wakiinuliwa kihuduma,basi wanasema yatosha.

~Wakisomea Biblia na kupata diploma, degree, masters ya teologia basi wanajiona kwamba wamemaliza yote.

👉Wakijuwa kuimba,kupiga guitar basi wanasema yatosha.Wala hawapendi kuomba ushauri kwa wazee,mzee akimshauri utasikia wewe mzee wakati wako umekwisha,tuachie vijana.
➡Ni kweli wakati wake umekwishapita lakini sikiliza ushauri,Maonyo yake akuambiayo.
Ewe kijana nakushauri kwa huruma zake Mungu acha kumdharau mzee,Bali muheshimu sana maana huyo ni adhina kubwa kwako mpendwa.

             1TIMOTHEO 4:11-12.

👉Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.

👉Mtu awayeyote asidharau ujana wako,Bali uwe kielelezo kwao waaminio,katika usemi na mwenendo,na katika upendo na imani na usafi.

➡Lakini vijana wengi tunadharaulisha ujana wetu kwa matendo yetu mabaya katika jamii,ndimi zetu zimejaa matusi tuuuu,hivi kwa mwenendo wako huo utakuwaje kielelezo kwa watu? Jirekebishe kijana mwenye tabia mbovu na mbaya,la sivyo utaeendelea kuudharaisha ujana wako,na imani yako inakuwa sio kitu.

➡Acha kuudharaulisha ujana wako wewe kijana mwenzangu.
Na wewe mzee wangu kichwa chako kinathamani kubwa sana endapo kitaonekana katika njia bora ambayo inampendeza Mungu, usiwe wewe mwenyewe ndio chanzo cha kujidharaulisha mbele ya vijana,vijana tunahitaji maonyo yako,tunahitaji ushauri wako ili tusonge mbele zaidi,hivyo thamanisha uzee wako lakini pia thaminisha kichwa chako chenye mvi.Wewe ni adhina kubwa kwetu sisi vijana,jitambue nakuambia.

👉Vijana wenzangu naomba niwashauri kwamba Tusiwaige wale vijana waliomdhiaki Mtumishi wa Mungu Elisha,hatimaye wakaliwa na Dubu;Bali tuwaige wale vijana waliomuinua Musa mikono yake; Tuishi pamoja na wazee wetu,tutachota mambo makubwa kutoka kwao.

➡Ushirika wetu na wazee nakuambia utakufanya uonekane kuwa ni kijana unayeifahaa jamaa ya waaminio na hata wasioamini pia,kwa mwenendo wako safi nakuambia utawavuta wengine kuja kwa Yesu Kristo ya kuziokoa nafsi zao na mauti.
~Tukae bega kwa Bega na wazee wetu Mungu atatufanikisha na kutuinua zaidi wapendwa.

➡Tusiwadharau wazee,tuwaheshimu sana,tuombe ushauri kwa wazee ndugu zangu Mungu atatufanikisha.
➡Tumia nguvu zako vema mpendwa maana nguvu zako ndio fahari yako.

👉Thamani ya ujana wako iko mikononi mwako,thamani ya UJANA wako ni nguvu zako, Tumia Nguvu zako vizuri.
➡Usitarajie kuheshimiwa kama wewe mwenyewe hujajiheshimu mpendwa.
➡Thaminisha,Heshimisha ujana wako ewe kijana mwenzangu.

👉Kijana Mungu anahitaji umtumikie siku za ujana wako mpendwa, kabla hazijaja siku mbaya kwako.
➡Chunguza Sana ujana  wako leo.
➡Unaandikiwa  wewe kijana Maana unazo nguvu, na NENO la BWANA linakaa ndani yako. Nawe utamshinda huyu shetani kwa nguvu za NENO La Mungu ndani yako.

👉Kijana Jaza NENO la Mungu moyoni mwako nalo NENO litakuongoza Katika njia ikupasayo.

Saturday, September 2, 2017

UKUU WA KRISTO NA KAZI ZAKE

      Wakolosai 1: 15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;
20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
21 Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa;
22 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;
23 mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.

        ¶Yesu Kristo siyo kiumbe kama nusu Malaika Bali ni
Mungu mwenyewe .

    ¶Mungu haonekani lakini tunaweza kumuona na kumjua kwa njia ya Yesu Kristo .

Yesu ni Mungu na hivyo hakuumbwa..

Alikuwepo kabla ya kuumbwa vitu vyote

Ni mkuu kuliko viumbe vyote.

Yeye mwenyewe ni Muumbaji ..

Ni  asili na mtawala wa Vitu vyote ..

Vinavyoonekana na visivyoonekana pamoja na Ulimwengu wote  wa  Kiroho yaani wa  viumbe wa Malaika

¶Yesu Kristo ni  kusudi na lengo la  viumbe vyote

Viumbe vyote vipo kwa ajili ya Utukufu wake (16-17)

            Yesu Kristo ana uungu wa  milele ndani yake  unaomfanya kuwa asili na kichwa cha Viumbe vyote vionekanavyo .

       Yesu Kristo ni  asili na kichwa cha Uumbaji mpya yaani Kanisa kwa sababu ya USHINDI WA UFUFUO WAKE .

       YESU KRISTO ni  mtawala mkuu ..Hana mchanganyiko wa  Mungu na Malaika Bali katika nafsi yake  mwenyewe ana hali  kamili na Uwezo wa  Uungu ( 18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;)

       
         Yesu Kristo ni  mpatanishi wa wenye dhambi ..Kwa njia ya kifo chake watu tunarudishwa katika hali ya Amani na mapatano na Mungu (Verse 20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni).

       Sisi kama wakristo kama ilivyokuwa kwa wakolosai walivyoona /tulivyoona nguvu ya Mungu katika maisha yao /yetu  tumeokolewa katika dhambi zetu .

Wokovu wetu umetokana na Kristo mwenyewe aliyefanyika mwanadamu mwenye mwili kama sisi naye  amezichukua dhambi zetu nasi tumewekwa huru  mbali na dhambi na hukumu ya Milele .

       Nguvu ya malaika ama mwanadamu au kitu chochote haziwezi kuongeza jambo lolote katika hayo yaliyofanywa na Kristo .
21 Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa;
22 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;
23 mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.

      Ili  tuweze kusimama mbele za Mungu katika ukamilifu wa  Kristo ni  lazima tushikamane sana na ukweli wa Kristo..

   Tunapaswa kutambua kwamba kazi ya Kristo imekamilika ..

Ukweli wake upo  katika msingi wa Injili mahali popote injili inapohubiriwa wala haiwezi kubadilishwa ili ifae kwa mawazo Fulani za kibinadamu ...

     Yesu Kristo ni  yeye yule Jana leo na hata  milele .

Mungu akubariki kwa Ujumbe huu mfupi  Jumapili ya Leo

Na

Zawadi Ngailo

Sikonge Tabora

©2017
Contact
. http://ishineno.blogspot.com/

       https://m.facebook.com/maishaneno/

https://m.facebook.com/groups/166019753924509?view=permalink&id=226923244500826

http://zawadingailomedia.blogspot.com

https://m.facebook.com/zawadifngailo/

Friday, September 1, 2017

ARISE AND PRAY

"I am the LORD thy God, which brought thee out of the land of Egypt: open thy mouth wide, and I will fill it. (Psa 81:10)

IF ONLY YOU WOULD PRAY

Result Oriented Prayers

Rest Orchestrating Prayers

Reproach Overcoming Prayers

Real Offensive Prayers

Record Opening Prayers
Resistance Obviating Prayers

Revelation Obtaining Prayers
Rapid Outcome Prayers

Relevant On-point Prayers

Regular Obligatory Prayers...

New Things Would Begin In Your Life.

Arise And Pray.

            

SOMO :TENGENEZA MLANGO WA MUNGU KUINGIA KWENYE SHIDA YAKO

         BWANA YESU ASIFIWE
Mpendwa Zipo shida nyingi sana katika Maisha yetu ambazo mlango wake wa kutokea ni YESU Kristo peke yake
       Kitabu cha Ufunuo 3:20 kinasema hivi .."
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

       YESU Kristo anasema tazama Nasimama mlangoni ,Nabisha ,MTU akisikia sauti Yangu na kuufungua mlango ,Nitaingia kwake nami nitakula pamoja naye ,Na yeye pamoja nami .

            Mlango waweza kuwa ni moyo wako ,Mwili wako waweza kuwa mlango ,Familia ,Ukoo na ndugu zako vinaweza kuwa Mlango wa kuleta Shida /matatizo katika Maisha yako ..

                YESU Kristo amesimama mlangoni ( Kwenye familia yako ,Moyo wako katika ya Ukoo na ndugu zako ikiwa utaruhusu aingie mahali hapo atafanya mabadiliko yake juu ya watu wote na kila jambo lililopo mahali hapo ..

          IPO milango mingi lakini sisi tunayo mamlaka ya Ya kufungua na kufunga hiyo milango

Mathayo 16:19 " Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni."

      Yesu Kristo ametupa funguo za  mamlaka ya Ufalme wa Mhinguni ambazo zinatusaidia sisi kufunga na kufungua milango ya Shida mbalimbali katika Maisha yetu.

AINA YA UFUNGUO

1:UFUNGUO WA TOBA.

Rejea 2 Nyakati 7:14
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

      Toba inabadilisha uchumi na tabia ya mtu binafsi na nchi kwa Ujumla.
  Toba inafanya  tuombe na kusikilizwa na Mungu. .

Inatufanya tuache njia mbaya ..

Inatufanya tusamehewe dhambi zetu.

2Wakorintho 10:4
4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.

   Tunaangusha ngome kwa kuomba Toba

Ukitenda dhambi itakupeleka utumwani ,Mfano Magonjwa ,Uchumi kuyumba  ,ulevi

       Ili Mungu ajibu maombi yetu lazima akusamehe kwanza.

Toba /Kutubu ni kuomba msamaha kwa Mungu na kuonesha kwamba unahitaji msaada wa Mungu

Yeremia 29:1 Maneno haya ndiyo maneno ya waraka, ambao nabii Yeremia aliupeleka toka Yerusalemu, kwa hao waliobaki wa wakuu waliochukuliwa mateka, na kwa makuhani, na kwa manabii, na kwa watu wote, ambao Nebukadreza aliwachukua mateka toka Yerusalemu hata Babeli.

Mungu akubariki kwa somo hili fupi

Zawadi Ngailo
P.o box 124

Sikonge TABORA

+2556231 32 195

MAISHA NA NENO LA MUNGU

   
   

KIOO CHA NG'AMBO

KIOO CHA NG'AMBO

Matendo 28:3

[3]Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzonga-zonga mkononi.

Moto pekee ndio unaweza kutoa nyoka aliye katikati ya kuni

Naamini una mipango mizuri pamoja na maamuzi mema juu ya jambo fulani, lakini katika mipango na maamuzi hayo kuna nyoka(maumivu) ndani yake

Neno la Mungu(Moto) ndilo linaweza kupima uzuri wa maamuzi na mipango yako na kuondoa nyoka(maumivu) ndani yake

Mipango na maamuzi yako yasipite neno la Mungu(1wakor 4:6)

Ubarikiwe. ...

Na Tuvuke Mpaka Ng'ambo