Saturday, September 2, 2017

UKUU WA KRISTO NA KAZI ZAKE

      Wakolosai 1: 15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;
20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
21 Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa;
22 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;
23 mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.

        ¶Yesu Kristo siyo kiumbe kama nusu Malaika Bali ni
Mungu mwenyewe .

    ¶Mungu haonekani lakini tunaweza kumuona na kumjua kwa njia ya Yesu Kristo .

Yesu ni Mungu na hivyo hakuumbwa..

Alikuwepo kabla ya kuumbwa vitu vyote

Ni mkuu kuliko viumbe vyote.

Yeye mwenyewe ni Muumbaji ..

Ni  asili na mtawala wa Vitu vyote ..

Vinavyoonekana na visivyoonekana pamoja na Ulimwengu wote  wa  Kiroho yaani wa  viumbe wa Malaika

¶Yesu Kristo ni  kusudi na lengo la  viumbe vyote

Viumbe vyote vipo kwa ajili ya Utukufu wake (16-17)

            Yesu Kristo ana uungu wa  milele ndani yake  unaomfanya kuwa asili na kichwa cha Viumbe vyote vionekanavyo .

       Yesu Kristo ni  asili na kichwa cha Uumbaji mpya yaani Kanisa kwa sababu ya USHINDI WA UFUFUO WAKE .

       YESU KRISTO ni  mtawala mkuu ..Hana mchanganyiko wa  Mungu na Malaika Bali katika nafsi yake  mwenyewe ana hali  kamili na Uwezo wa  Uungu ( 18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;)

       
         Yesu Kristo ni  mpatanishi wa wenye dhambi ..Kwa njia ya kifo chake watu tunarudishwa katika hali ya Amani na mapatano na Mungu (Verse 20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni).

       Sisi kama wakristo kama ilivyokuwa kwa wakolosai walivyoona /tulivyoona nguvu ya Mungu katika maisha yao /yetu  tumeokolewa katika dhambi zetu .

Wokovu wetu umetokana na Kristo mwenyewe aliyefanyika mwanadamu mwenye mwili kama sisi naye  amezichukua dhambi zetu nasi tumewekwa huru  mbali na dhambi na hukumu ya Milele .

       Nguvu ya malaika ama mwanadamu au kitu chochote haziwezi kuongeza jambo lolote katika hayo yaliyofanywa na Kristo .
21 Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa;
22 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;
23 mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.

      Ili  tuweze kusimama mbele za Mungu katika ukamilifu wa  Kristo ni  lazima tushikamane sana na ukweli wa Kristo..

   Tunapaswa kutambua kwamba kazi ya Kristo imekamilika ..

Ukweli wake upo  katika msingi wa Injili mahali popote injili inapohubiriwa wala haiwezi kubadilishwa ili ifae kwa mawazo Fulani za kibinadamu ...

     Yesu Kristo ni  yeye yule Jana leo na hata  milele .

Mungu akubariki kwa Ujumbe huu mfupi  Jumapili ya Leo

Na

Zawadi Ngailo

Sikonge Tabora

©2017
Contact
. http://ishineno.blogspot.com/

       https://m.facebook.com/maishaneno/

https://m.facebook.com/groups/166019753924509?view=permalink&id=226923244500826

http://zawadingailomedia.blogspot.com

https://m.facebook.com/zawadifngailo/

No comments:

Post a Comment