Wednesday, September 6, 2017

KUBEBEANA MIZIGO

.          ”Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri Zake.”_ (Danieli 9:3, 4).*

Akiwa na mzigo kwa niaba ya Israeli, Danieli alijifunza upya unabii wa Yeremia. Ulikuwa waziwazi kiasi ambacho kwenye vitabu alielewa shuhuda hizi zilizorekodiwa “hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.”

Kwa imani ambayo msingi wake ulikuwa kwenye neno la unabii lililo imara zaidi, Danieli alimsihi Bwana kwa ajili ya kutimizwa upesi kwa unabii huu. Alisihi kwa ajili ya heshima ya Mungu kudumishwa. Katika ombi lake alijiweka yeye mwenyewe kikamilifu pamoja na wale waliokuwa wamepungua katika makusudi ya Mungu, akiungama dhambi zao kana kwamba ni zake mwenyewe.

Ombi lililotoka kwenye midomo ya Danieli lilikuwa la ajabu sana! Linadhihirisha nafsi iliyonyenyekea kiasi cha ajabu! Joto la moto wa kimbingu lilitambulika katika maneno yaliyokuwa yakipanda juu kwa Mungu. Mbingu ilijibu ombi lile kwa kumtuma mjumbe wake kwa Danieli. Katika siku zetu hizi, sala zinazowasilishwa namna hiyo zitashinda pamoja na Mungu. “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana.”

Kama ilivyokuwa nyakati za kale, ombi lilipotolewa, moto ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza kafara iliyokuwa juu ya madhabahu; hivyo, kama majibu kwa ajili ya maombi yetu, moto wa kimbingu utakuja kwenye roho zetu. Nuru na uwezo wa Roho Mtakatifu vitakuwa vyetu. Je, sisi hatuna hitaji kubwa la kumwita Mungu kama alivyokuwa Danieli? Ninanena na wale wanaoamini kwamba tunaishi kwenye kipindi cha mwisho kabisa cha historia ya dunia hii. Ninawasihi mbebe mioyoni mwenu mzigo kwa ajili ya makanisa yetu, shule zetu na taasisi zetu.

Mungu yule aliyesikia maombi ya Danieli atasikia maombi yetu tunapomjia kwa moyo wa toba. Mahitaji yetu ni ya muhimu pia, matatizo yetu ni makubwa na tunahitaji kuwa na makusudi yenye mkazo uleule, na kwa imani tumtwike mzigo wetu yeye aliye Mbeba-mizigo mkuu. Lipo hitaji kwa ajili ya mioyo kuguswa sana wakati wetu kama ilivyokuwa wakati Danieli alipoomba.

No comments:

Post a Comment