Tuesday, September 5, 2017

FAHARI YA KIJANA NI NGUVU ZAKO

Bwana Yesu Kristo atukuzwe wana wa Mungu aliye hai.
Ninazidi kumshuru Mungu kwa ulinzi wake na kuzidi kutukutanisha tena, jina la Bwana lihimidiwe.

Karibu sana mpendwa tusemezane katika ujumbe huu wa neno la Mungu ambao Roho wa Mungu ametupatia.

Ujumbe:FAHARI YA KIJANA NI NGUVU ZAKO.
               ======================

Katiika ujumbe wetu naomba kuzungumza na kusemezana na vijana wote wa kike na wa kiume,na labda Roho wa Mungu atasema nawe hata kama sio kijana basi naomba ulipokee neno hilo litakusaidia.

         Tusome MITHALI 20:29

Fahari ya kijana ni nguvu zao;Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.

Nguvu
---------- Ni uwezo unaomsababisha mtu kufanya jambo Fulani katika maisha yake.

➡Hizo nguvu ambazo unazo wewe kijana,naomba nikuambie kwamba Mungu hajakupa nguvu hizo kwa ajili ya:
👉Kuiba,kubaka,kubomoa nyumba za watu,wala hujapewa nguvu hizo kwa ajili ya kupiga watu,wala sio za kutukana wazee mitaani.

👉Bali  Mungu amekupa nguvu hizo kwa ajili ya kumtumikia,kwa ajili ya kufanya kazi nzuri za mikono yako naye akubariki,kwa ajili ya kuwasaidia wengine mpendwa.
➡Hivyo Tumia nguvu ulizonazo leo kumtumikia Mungu wako kijana wangu.

👉Lakini vijana wengi Leo tunazitumia hizo nguvu zetu vibaya sana nakuambia mpendwa; wengine wanazitumia kuvuta madawa ya kulevya,wengine kuiba,wengine kubaka mitaani,wengine kupigana,wengine kutukana watu.

➡Nakuambia wewe kijana utumiaye nguvu zako vibaya wakati wa ujana wako,nakuambia siku inakuja ambayo utazitafuta nguvu hizo.
➡Wengine husema siwezi kumtumikia Mungu nikiwa kijana,Bali nitamtumikia Mungu nikiwa mzee,hivi calender ya maisha yako unayo wewe mikononi mwako?.

      Soma hii hapa MHUBIRI 12:1-2

1⃣Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako,Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,Wala haijakaribia miaka utakaposema,Mimi sina furaha katika hiyo.

2⃣Kabla jua,Na nuru na mwezi,na Nyota havijatiwa Giza;Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;....

👉Unaona hapo 👆wewe kijana mwenzangu;neno linakuambia tumkumbuke Muumba wetu ambaye ni Mungu wetu katika siku za ujana wetu,kumbuka  kumtumikia BWANA Eee kijana .
➡Nakushangaa wewe unayesema kwamba unasubiri uwe mzee ndio utamtumikia Mungu.

👉Siku zinakuja wewe kijana ambazo hizo nguvu zako unazoziaribu Leo utazitafuta nakuambia.
➡Mungu anataka tumtumikie Maishani mwetu tukiwa bado tuna nguvu wapendwa.
➡Usisubiri umekuwa mgonjwa ndio sasa unakumbuka Mungu yupo,jitambue bado usiku haujakufikia mpendwa.

👉Acha kutumia nguvu zako kuwatukana wazee nakuambia kijana mwenzangu.Wewe ujajivunia huo ujana wako na kuanza kuwadharua na kuwatukana wazee,nakuambia huyo mzee unayemtukana na kumdharau alikuwa kijana kama wewe.

👉Yaani kinywa chako kimejaa matusi,maneno machafu dhidi ya wazee,nakuambia ole kwako.
➡Unajivunia nguvu zako kwa kuvuta bangi,naomba nikuambie kwamba hata na huyo mzee nguvu alikuwa nazo.

Wahenga walisema kwamba:
➡Kuishi kwingi ni kuona mengi√.
Sasa wewe huyo mzee unayemdharau alishayaona mengi sana,je utaomba ushauri kwake? Muheshimu mzee mpendwa kijana.

➡Tambua kwamba Wewe sio wa kwanza kuwa kijana,wapo waliokutangulia wewe ambao waliwaheshimu wazee wao na maisha yao yakawa mazuri sana,na Mungu akawafanikisha na kuwainua zaidi.

      Ona vijana hawa:

👉Kijana Yoshua alimuheshimu sana Musa,na baada ya kifo cha Musa Mungu akamuinua Yeye.

👉Kijana Samweli alimuheshimu sana Eli na akawa kijiana mwenye maadili mema,na Mungu akamtumia zaidi.

👉Kijana Timotheo alimuheshimu Paulo.
Na wengine wengi mpendwa ambao waliwaheshimu wazee wao;waliyasikiliza mausi,ushauri na maonyo yao, na Mungu akawainua zaidi na zaidi;kwanini wewe unamdharau mzee huyo?

👉Ni kweli kwamba Mungu ameiweka huduma kubwa ndani yako,lakini tambua unahitaji ushauri wa wazee ili uzidi kusonga mbele zaidi;acha kuwadharau na kuwatukana ewe kijana mwenzangu.

Jambo la kusikitisha ni kwamba:

➡Vijana wengi makanisani wakiinuliwa kihuduma,basi wanasema yatosha.

~Wakisomea Biblia na kupata diploma, degree, masters ya teologia basi wanajiona kwamba wamemaliza yote.

👉Wakijuwa kuimba,kupiga guitar basi wanasema yatosha.Wala hawapendi kuomba ushauri kwa wazee,mzee akimshauri utasikia wewe mzee wakati wako umekwisha,tuachie vijana.
➡Ni kweli wakati wake umekwishapita lakini sikiliza ushauri,Maonyo yake akuambiayo.
Ewe kijana nakushauri kwa huruma zake Mungu acha kumdharau mzee,Bali muheshimu sana maana huyo ni adhina kubwa kwako mpendwa.

             1TIMOTHEO 4:11-12.

👉Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.

👉Mtu awayeyote asidharau ujana wako,Bali uwe kielelezo kwao waaminio,katika usemi na mwenendo,na katika upendo na imani na usafi.

➡Lakini vijana wengi tunadharaulisha ujana wetu kwa matendo yetu mabaya katika jamii,ndimi zetu zimejaa matusi tuuuu,hivi kwa mwenendo wako huo utakuwaje kielelezo kwa watu? Jirekebishe kijana mwenye tabia mbovu na mbaya,la sivyo utaeendelea kuudharaisha ujana wako,na imani yako inakuwa sio kitu.

➡Acha kuudharaulisha ujana wako wewe kijana mwenzangu.
Na wewe mzee wangu kichwa chako kinathamani kubwa sana endapo kitaonekana katika njia bora ambayo inampendeza Mungu, usiwe wewe mwenyewe ndio chanzo cha kujidharaulisha mbele ya vijana,vijana tunahitaji maonyo yako,tunahitaji ushauri wako ili tusonge mbele zaidi,hivyo thamanisha uzee wako lakini pia thaminisha kichwa chako chenye mvi.Wewe ni adhina kubwa kwetu sisi vijana,jitambue nakuambia.

👉Vijana wenzangu naomba niwashauri kwamba Tusiwaige wale vijana waliomdhiaki Mtumishi wa Mungu Elisha,hatimaye wakaliwa na Dubu;Bali tuwaige wale vijana waliomuinua Musa mikono yake; Tuishi pamoja na wazee wetu,tutachota mambo makubwa kutoka kwao.

➡Ushirika wetu na wazee nakuambia utakufanya uonekane kuwa ni kijana unayeifahaa jamaa ya waaminio na hata wasioamini pia,kwa mwenendo wako safi nakuambia utawavuta wengine kuja kwa Yesu Kristo ya kuziokoa nafsi zao na mauti.
~Tukae bega kwa Bega na wazee wetu Mungu atatufanikisha na kutuinua zaidi wapendwa.

➡Tusiwadharau wazee,tuwaheshimu sana,tuombe ushauri kwa wazee ndugu zangu Mungu atatufanikisha.
➡Tumia nguvu zako vema mpendwa maana nguvu zako ndio fahari yako.

👉Thamani ya ujana wako iko mikononi mwako,thamani ya UJANA wako ni nguvu zako, Tumia Nguvu zako vizuri.
➡Usitarajie kuheshimiwa kama wewe mwenyewe hujajiheshimu mpendwa.
➡Thaminisha,Heshimisha ujana wako ewe kijana mwenzangu.

👉Kijana Mungu anahitaji umtumikie siku za ujana wako mpendwa, kabla hazijaja siku mbaya kwako.
➡Chunguza Sana ujana  wako leo.
➡Unaandikiwa  wewe kijana Maana unazo nguvu, na NENO la BWANA linakaa ndani yako. Nawe utamshinda huyu shetani kwa nguvu za NENO La Mungu ndani yako.

👉Kijana Jaza NENO la Mungu moyoni mwako nalo NENO litakuongoza Katika njia ikupasayo.

1 comment: