Wednesday, January 25, 2017

KUISHI KWA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU

Kuishi kwa Kuongozwa na Roho Mtakatifu Language Swahili (Wagalatia 5:16-25)

Utangulizi: Hakuna Mkristo mkomavu anayeamini kwamba imani ndio jibu la mwisho la “ni kwa jinsi gani tunapaswa kuishi?” Kufikiri na kutenda vinaendana. Hakuna Mkristo wa dhati anatakayedai kuwa kutembea na Mungu ni jambo rahisi. Wakristo wengi ninaowafahamu kimsingi wanasema, “Ninaokolewa kwa neema pekee. Kwa sababu ya upendo wangu kwa Mungu, ninafanya uamuzi wa kutembea nae na kuyafanya/kuyatenda mapenzi yake.” Nilipojaribu kuwauliza zaidi waliongezea kwa kusema, “Na, kama mtu hatembei pamoja na Mungu, hiyo inaonyesha kuwa hawana imani.” Ama kwa hakika, wale “Wakristo” wanaotumia imani kama kisingizio cha kuishi maisha ya kiovu hawaielewi injili. Lakini, baadaye, nimekuwa nikilitafakari zaidi suala hili kuhusiana na jinsi gani Mkristo anayeokolewa kwa neema anavyopaswa kuenenda katika maisha yake ya kila siku. Hebu tuzame kwenye Biblia yetu na kuona kile ambacho Paulo anatufundisha kuhusiana na maisha ya kila siku! Mzozano/Ugomvi Tunahitaji kupata muktadha, kwa hiyo kwanza kabisa hebu soma kwa haraka Wagalatia 5:16-21. Je, hii inatuambia nini kuhusu neema na kuishi maisha sahihi? (Kama unaishi maisha yenye ubinafsi, maovu, yasiyo makamilifu, hutakwenda mbinguni.) Huyu ni Paulo anayeandika haya! Je, hii inatenda kitu gani kwenye fikra zetu kuhusu neema? (Inamaanisha kuwa mwisho wa neema hauwezi kuwa ni tabia ya kiovu.) Majuma mawili yaliyopita tulijifunza kuwa “mchakato” wa Sara kutimiza lengo la Mungu (kwamba Ibrahim atakuwa na uzao) uliishia kwenye balaa kubwa sana. Je, hakuna tunachoweza kukifanya (au tunapaswa kukifanya) ili tujihusishe kwenye kuishi maisha sahihi? Je, hilo litakuwa ni “mpango wa Sara,” yaani, kosa la “kuhesabiwa haki kwa matendo?” Hebu tuyaangalie haya mafungu kwa undani zaidi. Soma Wagalatia 5:16. Je, inamaanisha nini “kuishi kwa kuongozwa na Roho?” (Ishi kwa mujibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu.) Soma Wagalatia 5:17. Je, hili suala la kuishi kwa kuongozwa na Roho linatendeka? Kama umesema kuwa, “Ndiyo,” je, unaielezeaje kauli ya Paulo kwamba “hamfanyi yale mnayoyataka?” (Inaweza kumaanisha kuwa mnataka kufanya jambo jema, lakini badala yake mnafanya uovu. Pia inaweza kumaanisha mna matamanio ya asili ya kutenda uovu, lakini kwa sababu ya Roho Mtakatifu, badala yake mnatenda jambo jema. Hii maana ya pili inaendana na kile tulichokisoma hivi punde katika fungu la 16.) Soma Warumi 7:21-25. Je, Paulo anazungumzia tu kuhusu watu wabaya? Au, je, anamzungumzia tu wewe na mimi? (Paulo anajizungumzia yeye mwenyewe. Anazungumzia kuhusu Wakristo “wazuri.” Sote tuna asili ya dhambi. Sote tunavutwa kuishi kwa mujibu wa asili hiyo. Tunajikuta tunatenda uovu ambao hatutaki kuufanya.) oma Wagalatia 5:18. Je, hii inamaanisha nini – sina haja ya kuwa na wasiwasi juu ya kile ambacho sheria inakisema? (Haiwezi kumaanisha hivyo, kwani hivi punde tu umesoma kuwa watenda maovu hawatakwenda mbinguni. Hitimisho la pekee la kimantiki ninaloweza kulifikia ni kuwa tuna chaguzi mbili. Tunaweza kuongozwa na Roho Mtakatifu au tunaweza kuongozwa na asili yetu ya dhambi.) Je, hii inapendekeza kuwa kwa namna fulani hivi sheria inahusianishwa na asili yetu ya dhambi? (Soma Warumi 7:8-10. Paulo anasema kuwa sheria inachokonoa tabia ya kidhambi. Hii sio ya kawaida, kwa hiyo tunahitajika kulichunguza hili zaidi.) Kuishi kwa mujibu wa Sheria ijui jinsi ya kuwa na mjadala thabiti wa hili suala bila kuzungumzia dhambi mahsusi. Kwa hiyo, hebu tuzungumzie kuhusu kisa mahsusi kuhusiana na dhambi mahsusi. Soma 2 Samweli 11:1-4. Nimefundisha kisa hiki mara nyingi, nimehubiri kuhusiana nacho. Kama wewe ndiye ungekuwa Daudi, na ukataka kuepuka hii dhambi, je, ni hatua gani za kivitendo ambazo ungezichukua? (Kile ambacho mara zote nimekuwa nikikisema huko nyuma ni kwamba Daudi alikuwa anachukua mfululizo wa hatua kuelekea kwenye dhambi. Baadhi ya hatua zinaweza zisiwe dhambi, lakini bado zilimwelekeza kwenye uelekeo wa dhambi.) Je, hizi hatua mbaya zinaweza kuwa zipi? (a. Kutokwenda vitani na majeshi yake; b. Kumwangalia Bathsheba kwa muda mrefu; c. Kuvutiwa/kupendezewa nae; d. Kutuma apelekewe hata ingawaje alijua kuwa alikuwa ameolewa; na hatimaye kufikia ukomo wa dhambi, e. Kufanya uzinzi.) Kama wewe (namaanisha wewe binafsi) ulitaka kuepuka uzinzi, je, ungeepuka kuchukua hizi hatua? (Ndiyo. Hii inaleta mantiki. Lakini, nadhani kwamba nimekuwa nikifundisha kwa kutumia njia isiyo sahihi. Kiini cha hatua ni sheria. Kiini cha hatua ni uzinzi na jinsi ya kutousogelea kwa ukaribu sana. Kuilenga dhambi na sheria ni njia ya kuhesabiwa haki kwa matendo.” Ninaiangalia asili yangu ya dhambi na ninatafakari jinsi ya kuishinda. Kama Sara, mimi ni mhandisi wa nini cha kufanywa ili kutimiza lengo la Mungu.) Je, onyo la kivitendo la Paulo kuhusu kuhesabiwa haki kwa imani ni lipi? (Halifanyi kazi. Katika Warumi 7:5 Paulo anasema kuwa sheria inaamsha matamanio yetu ya kidhambi. Wagalatia 5:3 inapendekeza kuwa haiwezekani kuitimiza sheria. Katika Wagalatia 5:4 Paulo anaeleza kuwa njia ya matendo inashindwa kwa sababu inamwondoa Mungu kutoka kwenye mpambano.) Je, kuna chochote tunachoweza kukifanya ili kuendeleza tabia zetu wenyewe? Hebu tubaini hilo katika sehemu inayofuatia. . Kuishi kwa mujibu wa Roho oma Wagalatia 5:22-23. Je, ni kwa jinsi gani kuishi kwa mujibu wa Roho kunatofautiana na kuishi kwa mujibu wa sheria? (Unazingatia masuala chanya, hauzingatii masuala hasi. Hauelekezi hatua zako kuelekea dhambini, unaelekeza hatua zako kuelekea kwenye haki.) Hebu turejee kwenye mfano wetu wa msingi wa Daudi. Kama umeamua kuacha kuwafundisha akina Daudi wa siku zijazo kuziangalia hatua zao, kuacha kuziangalia “taa nyekundu” za kimaadili, sasa utakuwa unawafundisha kitu gani? (Vipi kama badala yake tungesema “Mtizamie/mwangalie mkeo. Leta upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi kwenye maisha ya mkeo. Usiziangalie ‘taa nyekundu.’”) Hebu turejee tena kitu fulani tulichojadili juma lililopita. Soma Wagalatia 5:14-15. Hili ndilo lengo la maisha yanayoongozwa na Roho. Je, Daudi angepaswa kuwa anajiuliza kuhusu kitu gani, badala ya kuuliza “Ni hatua gani za kuielekea dhambi (Bathsheba) ninazopaswa kuziepuka?” (Je, ninaweza kufanya jambo gani ili niweze kumfurahisha mke wangu? Je, ninaweza kufanya jambo gani ili niweze kumfurahisha Mungu wangu? Je, ninaweza kufanya jambo gani ili niweze kumsaidia mke wangu? Je, jukumu hili linapendeza mbele za Mungu wangu na mke wangu? Je, hii inakusaidia kuelewa kile anachokimaanisha Paulo anapoandika “kama unaongozwa na Roho, haupo chini ya sheria?” (Roho anauliza, “je, nifanye nini ili niweze kumpenda Mungu na mwenzi wangu?” Sheria inasema, “Je, ninapaswa kufanya nini ili niweze kuuepuka uzinzi?” Lengo ni lile lile – kuwa mwaminifu kwa mwenzi wako. Kama vile Sara na Mungu walivyokuwa na lengo moja – kuwapata wazao kwa ajili ya Ibrahim. Ni mchakato, njia ya kulielekea lengo, linalowatenganisha wale wanaoamini katika kuhesabiwa haki kwa imani na wale wanaoamini katika kuhesabiwa haki kwa matendo.) Wagalatia 5:13 inapotualika “kuwatumikia” wengine, na Wagalatia 5:22 inapotuambia kuwa tunda la kwanza la kuishi maisha yanayoongozwa na Roho ni “upendo,” je, hii inatuambia nini kuhusu kujitazamia wenyewe, ubinafsi, “kutizama kitovu?” (Mambo haya ni makosa.) Je, kuna funzo katika jambo hili kwa ajili yetu kuhusu jinsi ambavyo tunapaswa kutembea na Mungu? (Rafiki, natumaini kwamba unaweza kuona kuwa kuitazamia sheria, kuzitazamia “taa nyekundu” ni kujitazamia mwenyewe. Je, ninaendeleaje? Kutazamia kumpenda Mungu na wenzi wetu na wengine kunafikia kwenye swali, “Je, vinaendeleaje? Je, ninavifurahisha?) Soma Wagalatia 5:24. Je, njia yetu ya kukabiliana na asili yetu ya dhambi inapaswa kuwa ipi? (Tunataka ife! Je, unaweza kuona tena kuwa ni makosa kwa kiasi gani kuzitazamia asili zetu za dhambi na kupima vipimo vyake kuielekea dhambi?) oma Wagalatia 5:25. Kama unataka kuendana hatua kwa hatua na mwanadamu mwingine, je, unahitajika kufanya nini? (Angalia jinsi mtu huyo alivyotembea.) Je, inamaanisha nini kuendana “hatua kwa hatua” na Roho? (Kumwangalia Mungu wetu na kile kinachompendeza.) Hebu turejee tena Wagalatia 5:24-25. Je, sheria bado ni ya muhimu? (Ndiyo. Kama Wakristo “wasio wakomavu” sheria inatufundisha kuwa tunamhitaji Mwokozi. Lakini, mara tunapoupata huo ujumbe, basi hatupo tena chini ya uangalizi wa sheria. Hatujiangalii tena sisi wenyewe, kujipima wenyewe dhidi ya sheria. Badala yake, tunamwangalia Mungu, huku tukiwa tukiongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu ili tuweze kumpendeza Mungu. Basi kinachomiminwa maishani mwetu ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi.) Kama unajiona kuwa wewe sio mvumilivu, je, unapaswa kulifanyia hilo kazi? (Hapana! Hauiangalii dhambi. Usiyaangalie matendo, na kwa ujumla kuenenda kama Sara alivyofanya. Kwa uwezo wa Roho wa Mungu, badala yake zingatia kumpenda mtu ambaye huna uvumilivu nae. Hiyo ndio njia ya neema. Hiyo ndio njia ya kuhesabiwa haki kwa imani.) Soma Wagalatia 5:26. Kwa nini tuwe na majivuno kwa kuishi maisha sahihi? (Kama lengo ni kwa jinsi gani tunaishinda dhambi, na kama hatuko macho sana, hili linaweza kutokea. Kama lengo letu ni kumpenda Mungu na wale wanaotuzunguka, kamwe hili haliwezi kutokea.) Rafiki, natumaini kwa sasa unaweza kuona kwamba haki kwa imani sio tu kuwa inatuokoa kwa neema ya Mungu, bali pia inatuambia jinsi ambavyo tunapaswa kuishi kila siku. Je, utaamua hivi sasa kuacha kuangalia na kuzitazamia “taa nyekundu” na kuanza kuangalia jinsi ya kumpenda na kumfurahisha Mungu?

MAISHA NA NENO LA MUNGU
WHATSAPP GROUP

No comments:

Post a Comment